MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Askari wa Jeshi La Uhifadhi Kusini Wakumbushwa Wajibu
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Askari wa Jeshi La Uhifadhi Kusini Wakumbushwa Wajibu
Habari

Askari wa Jeshi La Uhifadhi Kusini Wakumbushwa Wajibu

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Mwandishi wetu.
MAOFISA  na Askari wanaounda Jeshi la Uhifadhi (JU) Nyanda za Juu kusini wametakiwa kuzingatia misingi ya Sheria na Kanuni za Jeshi hilo katika utekelezaji wa majukumu yao sanjari na kuheshimu utawala wa sheria na haki za binadamu.
Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, anayeshughulikia Maliasili Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba akiwa kwenye ziara ya kukagua Utendaji kazi wa Askari na Watumishi wa Taasisi za TAWA, TANAPA na TFS wa Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa.
Kamishana Wakulyamba amesisitiza kuwa  nidhamu na Uadilifu katika kutekeleza majukumu ya kila siku ndiyo msingi mkuu wa askari wa uhifadhi katika kutunza na kulinda rasilimali za maliasili.
Akiwa kwenye Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, alitembelea Mapori ya akiba ya Rwafi na Uwanda Mkoani Rukwa, Pori la akiba la Rukwati Piti na Mpanga Kipengele Mkoani Mbeya yanayosimiwa na TAWA.
Aidha, katika ziara hiyo Kamishna Wakulyamba alipata nafasi pia ya kuzungumza na Askari wa TFS  Mkoa wa Mbeya, Askari wa mashamba ya Pori la Msitu wa Mbizi Mkoani Rukwa na Pori la Msitu wa Sao Hii Mkoani Iringa.
Maofisa na Askari hao walipata fursa ya kuelimishwa kupitia mada mbalimbali zilizojikita katika masuala ya  nidhamu, uadilifu na matumizi sahihi ya silaha sanjari na Misingi ya utawala wa Sheria na Haki za binadamu.
Mafunzo haya yaliyotolewa pia na maafisa kutoka Jeshi la polisi yaligusia kanuni sahihi na salama za  umiliki na utunzaji wa silaha, mambo ya kuepuka wanapokuwa na sillaha za moto na madhara yatokanayo na matumizi mabaya ya silaha.
“Sisi ni Askari wa Uhifadhi, na moja ya sifa na msingi mkuu wa Askari wa Jeshi lolote duniani ni Nidhamu na Uadilifu. Askari anapaswa kutekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na jamii inayozunguka Hifadhi kwa kusimamia mambo makubwa mawili ambayo ni nidhamu na Uadilifu” alisisitiza Kamishna Wakulyamba.
Akihitimisha ziara yake katika Ofisi za TAWA Makao Makuu ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mkoani Iringa, Kamishna Wakulyamba aliwataka Maofisa na Askari wa Uhifadhi kujiepusha na vitendo viovu ikiwemo, rushwa, ulevi wa kupindukia, kuwabambikia watu kesi au matukio ya uhalifu ya uongo na kuepuka matumizi ya nguvu yasiyo ya lazima.
Kamishna Wakulyamba alitumia ziara hiyo kusikiliza Kero za Askari na baadhi ya wananchi ambao ni wavuvi kwenye Pori la Akiba la Uwand pamoja na kukagua ujenzi wa majengo na miundombinu  mbalimbali ya Wazara hiyo.

You Might Also Like

Muhogo, viazi kuongezewa tija kwenye uzalishaji

Tutuba: Noti Mpya Kuanza Kutumika Februari Mosi mwaka huu

WDC Kuboresha Miradi Yake Ya Majengo

India Kuwekeza Katika Sekta Ya Nishati Nchini

Hali Ya Ulinzi Na Usalama Wa Mipaka Ni Salama

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TARI yapongezwa kwa kuwa na teknolojia bora za kilimo
Next Article Watumishi wa serikali watakiwa kutokuwa kikwazo kwa wawekezaji
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Ununuzi Wa Ndege Anga Za Kilimo Uanze Sasa-Bashe
Habari May 31, 2025
Wanafunzi Shule Ya Anlex, Walimu Wao Watinga Bungeni
Habari May 31, 2025
Ndege Ya TPHPA Yatua Rasmi Kudhibiti, Kwelea Kwelea, Viwavijeshi, Nzige 
Habari May 31, 2025
UDSM Yatafiti Ndege Nyuki ‘Drone’ Inayopunguza Uchafuzi Wa Hewa Ukaa
Habari May 29, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?