MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Asilimia 86.2 ya Wanawake  wanajishughulisha na shughuli za madini
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Asilimia 86.2 ya Wanawake  wanajishughulisha na shughuli za madini
Habari

Asilimia 86.2 ya Wanawake  wanajishughulisha na shughuli za madini

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
MATOKEO ya utafiti mdogo uliofanywa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa kushirikiana na Chama cha Wachimbaji Wanawake Tanzania (TAWOMA) umeonesha zaidi ya asilimia 80 ya wanawake kutoka  mikoa ya Shinyanga, Geita, Mara na Simiyu wanajishughulisha na Shughuli za sekta ya Madini nchini.
Hayo yamesemwa leo  na Naibu Waziri wa Madini  Dkt. Steven Kiruswa alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Viti maalumu vya wanawake Fatma Hassan aliyetaka kujua idadi ya  wanawake wanaomiliki migodi ya madini nchini.
Naibu Waziri amesema kuwa,  shughuli za madini nchini zinafanyika katika maeneo mbalimbali  kupitia watu binafsi na kampuni ambazo ndani yake kuna wanawake na wanaume.
Ameongeza kuwa, utafiti uliohusisha wanawake 992 umeonesha Wanawake 17 sawa na asilimia 1.7 wanamiliki migodi, wanawake 67 sawa na asilimia 6.8 wanamiliki maeneo ya uchimbaji (maduara) katika leseni za uchimbaji madini na wanawake 855 sawa na asilimia 8.2 wanajishughulisha na kazi zinazohusiana na uchimbaji pamoja na uchenjuaji madini huku wanawake 53 sawa na asilimia 5.3 wanatoa huduma maeneo ya uchimbaji.
Dkt. Kiruswa ameongeza kuwa  kulingana na umuhimu na mchango wanaotoa kwa taifa,  Serikali itaendelea kuwasimamia na kuwapatia leseni wanawake wanaojishughulisha na uchimbaji wa madini ili kuongeza mchango wao kwenye sekta pia kuimarisha uchumi wao.
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 ilibaini kuwa  kuna takribani wanawake milioni 3 wanaoshiriki katika mnyororo mzima wa thamani madini.

You Might Also Like

Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, Laleta Furaha Kwa Watoto

July 10, 2025

Miradi 10 Ya Kimkakati TPA Kuinua Uchumi

‘Jichunge’ Programu Ya Simu Yenye Mafanikio Katika Kuboresha Matumizi Ya Dawa Kinga Dhidi Ya VVU

Tume Ya Mipango Yaelekeza Waandishi Wa Habari Kutoa Elimu Ya Dira Ya Taifa Ya Maendeleo 2050

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TUGHE: Wafanyakazi wapewe haki ya kujiunga vyama vya wafanyakazi
Next Article Rais Samia kufungua kikao kazi cha watendaji serikalini
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Waziri Mkuu Majaliwa Akabidhi Tuzo kwa BoT Geita
Habari September 22, 2025
BoT Yarahisisha Uuzaji wa Dhahabu kwa Wachimbaji, Yatoa Punguzo La Mrabaha
Habari September 22, 2025
Waziri Mkuu Apongeza Huduma Kidijitali za NSSF, Maonesho Ya Madini Geita
Habari September 22, 2025
Mkuu Wa Mkoa Shinyanga Asifu Kazi Ya Bodi Bima Ya Amana
Habari September 22, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?