Na Danson Kaijage
DODOMA: JUMUIYA ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), itajadili Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali ( CAG), pamoja na kupitia agenda mbalimbali za kimaendeleo katika Mkutano Mkuu wa 39 wa mwaka.
Mwenyekiti wa ALAT, Murshid Ngeze amesema hayo alipozungumza na Waandishi wa Habari kuhusu maandalizi ya Mkutano huo ambao unatarajiwa kufanyika Jijini Dodoma. Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan.

“Katika mkutano huo pia tutajadili na kutathinini,kukichunguza katika utendaji wetu katika halmashauri.
“Kutoa taarifa za mapato na matumizi,kujua kila kata inapata kiasi gani cha fedha za maendeleo pamoja na kujua na kutoa majibu ambayo yalikuwa na Dukuduku,” amesema.
Pia amesema mkutano huo, utajadili na kupitisha bajeti sambamba na kueleza mapato na matumizi kwa lengo la kuweka uwazi kwa jamii.
Amesema pia watahuhisha jumuiya hiyo sambamba na kupitia utekelezaji wa kutaka kuanzisha ujenzi wa kitega uchumi kwe kiwanja chao chenye ukubwa wa mita za Mraba 6000.

Awali mkutano huo ulikuwa ufanyike Mwanza lakini sasa utafanyika Dodoma.