MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Takribani watu 200 Wamepata Ushauri Wa Kibingwa Wa Ubongo, Mifupa 
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Takribani watu 200 Wamepata Ushauri Wa Kibingwa Wa Ubongo, Mifupa 
Habari

Takribani watu 200 Wamepata Ushauri Wa Kibingwa Wa Ubongo, Mifupa 

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
GEITA: TAKRIBANI wananchi 200 wamepatiwa ushauri wa kitabibu kutoka kwa wataalamu wa Taasisi ya Mifupa na Tiba (MOI) katika maonesho ya Sekta ya madini yanayoendelea mkoani Geita.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Mgongo kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa (MOI), Dkt. Kenneth Mgidange, amesema idadi kubwa ya wananchi wamejitokeza kupata ushauri wa kiafya kuhusu matatizo ya mifupa, ubongo, na mgongo katika banda la taasisi hiyo.
Habari Picha 9578
“Tumeona muitikio mkubwa wa wananchi, ambapo takribani watu 200 wamehudumiwa kwa siku kadhaa za maonesho haya. Wengi wao walihitaji ushauri wa kitaalamu, na baadhi tumewashauri kufanya vipimo zaidi katika hospitali zao za karibu,” amesema Dkt. Mgidange.
Ameeleza kuwa huduma zinazotolewa na MOI ni pamoja na upasuaji wa ubongo, kuondoa uvimbe kupitia njia ya pua, upasuaji wa mgongo kwa kutumia matundu madogo, na upasuaji wa magoti kwa teknolojia ya kisasa inayoongozwa na akili bandia.
Habari Picha 9580
Dkt. Mgidange amesema: “Huduma za MOI ni za kibingwa na hutolewa kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu. Wananchi wa Geita na mikoa mingine wanahimizwa kufaidika nazo,”.
Aidha, wananchi wametakiwa kutumia mfumo wa kuweka miadi kwa njia ya mtandao kabla ya kufika MOI, ili kupunguza msongamano na muda wa kusubiri huduma, hasa kwa wagonjwa wanaosafiri kutoka mikoa ya mbali kama Geita.
Habari Picha 9581
Taasisi ya MOI ni miongoni mwa taasisi zinazoshiriki kwenye maonesho ya madini ya Geita kwa lengo la kutoa elimu ya afya na huduma kwa jamii, sambamba na kuwafikishia wananchi huduma za kibingwa nje ya Dar es Salaam.

You Might Also Like

Muswada kuja wa Watumishi Wanaofanya Kazi Eneo Zaidi ya Moja Kuanza kuchangiwa na Waajiri Wote

Tanzania Kujifunza Teknolojia Ya Magari Ya Umeme Singapore- Biteko

Waziri Mkuu Majaliwa ndani ya SGR

Rais Mwinyi Ajionea Mifumo Mbalimbali Banda La Ofisi Ya Waziri Mkuu Sabasaba

Kingalame Asisitiza Umuhimu wa Wachimbaji Kuuza Dhahabu Serikalini

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Taasisi za Elimu Geita Zatakiwa Kuanza Programu ya Maziwa Shuleni
Next Article Fursa za Uwekezaji Kanda ya Ziwa: Buzwagi na Maeneo Mengine ya Kimkakati
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Madaktari Kutoka Ireland Watoa Matibabu Ya Mifupa Kwa Watoto MOI
Habari October 20, 2025
Mwalim: Nikichaguliwa urais, Kigaila atakuwa Waziri Mkuu wangu
Habari October 20, 2025
ARTICLE 19,  JOWUTA KUSHIRIKIANA KUIMARISHA HAKI ZA WANAHABARI
Habari October 18, 2025
Profesa Ndunguru Aongoza Kikao Cha Mawaziri Wa DLCO- EA Akimwakilisha Bashe
Habari October 17, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?