WANANCHI wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora wamefurika uwanjani wakisubiri kwa hamasa kuwasili kwa Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 11,2025.

Dkt. Samia anaendelea na ziara za kampeni za uchaguzi mkuu mkoani Tabora akitokea Singida, ambapo leo anatarajia kufanya mikutano katika wilaya za Uyui, Urambo na Kaliua na kunadi sera na ahadi za Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa wananchi wa mkoa huo.
Imeandaliwa na Mwandishi wetu

