MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: REA Kusambaza Majiko Banifu 10,650 Mkoa Wa Pwani
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > REA Kusambaza Majiko Banifu 10,650 Mkoa Wa Pwani
Habari

REA Kusambaza Majiko Banifu 10,650 Mkoa Wa Pwani

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Mwandishi Wetu
WAKALA wa Nishati Vijijini (REA), umetoa jumla ya majiko banifu 10,650 mkoani Pwani ikiwa ni mwendelezo wa jitihada za Serikali za kuhakikisha  kila mwananchi anatumia nishati safi ya kupikia nchini.
Akizungumza leo Agosti 18, 2025 ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Meneja wa Teknolojia za Nishati kutoka REA,  Michael Kyessi amesema mradi huo unalenga kuuza na kusambaza Majiko Banifu kwa bei ya ruzuku ambapo mwananchi atachangia asilimia 20 ya gharama ya jiko huku asilimia 80 zikitolewa na Serikali.
Habari Picha 9036
“Mwananchi wa kawaida atachangia asilimia ishirini  tu za gharama za jiko ambapo bei ya jiko ni  sh 56,000 na mwananchi atagharamika kuchangia shilingi 11,200 tu baada ya ruzuku kutolewa na Serikali” amesema  Kyessi.
Pamoja na hilo  Kyessi amebainisha thamani ya mradi huo kwa ujumla ni  sh milioni 596,400,00 ambapo Serikali kupitia REA imetoa ruzuku ya sh milioni 477,120,00 ambayo ni sawa na asilimia 80.
Katika hatua nyingine, REA inatekeleza lengo la Serikali ya Tanzania kufikia mpango wa Umoja wa Mataifa wa “Nishati Endelevu kwa Wote” (SE4ALL) wa upatikanaji wa nishati
kwa asilimia 100 ifikapo mwaka 2030.
Habari Picha 9037
Mradi huo utatumia nishati Jadidifu ili kuweza kufikia wananchi wa maeneo ya visiwani na utekelezaji wake ni kwa kupitia mradi wa Ufadhili unaotegemea Matokeo (RBF) kupitia Benki ya Dunia.
“Serikali ya Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umetenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa kufunga mifumo ya umeme jua maeneo ya visiwani kwa kutoa ruzuku kwa bei ya mwisho ya mtumiaji wa mfumo wa Umeme Jua ili kufanikisha upatikanaji wa umeme katika maeneo hayo yaliyo mbali na Gridi ya Taifa, ” Amesema  Kyessi.
 Kyessi amesema katika Mkoa wa Pwani mradi wa umeme jua unategemea kuhudumia visiwa 13 na jumla ya watoa huduma wawili  wanategemea kuhudumia visiwa hivyo kupeleka jumla ya mifumo 2,243 ndani ya kipindi cha miaka miwili  na gharama za mradi kwa mkoa wa Pwani ni sh bilioni 1.372 ambapo ruzuku ni  milioni 935.7 sawa na asilimia 69 ya gharama zote ya mradi na sh milioni 436.6 ni fedha kutoka kwa wanufaika.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani  Abubakar Kunenge ameipongeza REA kwa mkakati wa kuendelea kuongeza matumizi ya Nishati safi na kuondoa kero kwa wananchi kuhusu matumizi ya kuni na mkaa ambayo ni hatarishi kwa afya zao.
Mradi huo utatekelezwa kwa muda wa miezi 15 katika mkoa wa Pwani na jumla ya Majiko Banifu 10,650 yatasambazwa kwa wananchi.

You Might Also Like

OUT yaunda Kamati ya Ufuatiliaji na Tathmini Mradi wa HEET

Tume ya Kurekebisha Sheria Yatoa Onyo Kali kwa Wanaovunja Sheria za Umwagiliaji

TEA Yawaalika Wananchi Kujifunza SDF Unavyofanya Kazi

Rais Samia kufungua mkutano wa Mawaziri wa Uvuvi

TASAC Yashuhudia Utiaji Saini  Mkataba Wa Uendeshaji Bandari Kavu Kwala

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Umoja, Mshikamano Vyatawala Mkutano Wa SADC
Next Article DKT. Biteko Azindua Mradi Utakaowakwamua Vijana Kiuchumi Katika Maeneo Yanayopitiwa Na Bomba La Mafuta Ghafi  (EACOP)
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Majaliwa Apongeza Jeshi La Magereza Kurasimisha Ujuzi Kwa Wafungwa
Habari August 27, 2025
Mapokezi Ya Katibu Mkuu CCM  Dkt Migiro CCM, Aahidi Ushirikiano
Habari August 27, 2025
Majaliwa Aagiza Kuimarishwa kwa Mafunzo ya Ufundi Stadi Nchini
Habari August 27, 2025
VETA Yaanzisha Kozi Mpya ya Teknolojia ya Mifumo ya Viwandani
Habari August 26, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?