MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Umoja, Mshikamano Vyatawala Mkutano Wa SADC
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Umoja, Mshikamano Vyatawala Mkutano Wa SADC
Habari

Umoja, Mshikamano Vyatawala Mkutano Wa SADC

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Mwandishi Wetu, 
Antananarivo: MKUTANO wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umehitimishwa jijini Antananarivo, Madagascar, Agosti 17, mwaka huu 2025, viongozi wakisisitiza umuhimu wa umoja, mshikamano na ushirikiano kama nyenzo kuu za maendeleo,
Ikiwa ni pamoja na kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazolikumba Bara la Afrika.
Habari Picha 9027
Tqarifa imesema katika mkutano huo, Tanzania iliwakilishwa na Makamu wa Rais, Dkt. Philip  Mpango, akimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan.
Aidha Uenyekiti wa jumuiya hiyo ulikabidhiwa rasmi kwa Madagascar kutoka kwa Zimbabwe.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, Mkutano huo ulihudhuriwa na wakuu wa nchi tisa, huku wakuu wa nchi wa Botswana, Namibia, Msumbiji na Mauritius wakihutubia kwa mara ya kwanza tangu wachukue madaraka.
Habari Picha 9031
Viongozi hao waligusia kwa kina masuala ya amani na usalama, ujenzi wa miundombinu, ukuaji wa uchumi, demokrasia na mtangamano wa kikanda.
Rais wa Zimbabwe,  Emmerson Mnangagwa, ambaye alikamilisha kipindi chake cha uenyekiti, ameeleza kuwa hali ya kisiasa katika ukanda wa SADC ni ya kuridhisha, isipokuwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambako bado kuna changamoto za kiusalama.
Amesisitiza kuwa migogoro inayoibuka barani Afrika inapaswa kutatuliwa na Waafrika wenyewe,  huku akieleza kuwa msaada wa nje unapaswa kuwa wa hiari na wa ziada tu.
Habari Picha 9021
Pia Viongozi wa SADC wamesisitiza umuhimu wa kukuza viwanda, kilimo, biashara na uongezaji thamani wa malighafi za ndani kama njia ya kuimarisha uchumi, kuongeza ajira na kipato hasa kwa vijana na wanawake.
Naye Rais wa Botswana, Duma Boko amesisitiza kuwa biashara baina ya nchi za Afrika ni njia madhubuti ya kujitegemea kiuchumi.
Katika eneo la miundombinu, nchi wanachama zilitakiwa kuharakisha utekelezaji wa miradi ya barabara, reli, nishati, maji na TEHAMA, ambayo imeainishwa katika Mpango Mkakati wa Maendeleo wa Kikanda wa mwaka 2030.
Vile vile nchi tisa, zikiwemo Tanzania, tayari zimesaini itifaki ya kuanzisha Mfuko wa Maendeleo wa Kikanda kwa ajili ya kugharamia miradi hiyo.
Mkutano huo ulitoa wito kwa nchi wanachama kuimarisha taasisi za kidemokrasia na kuhakikisha kuwa Uchaguzi Mkuu katika nchi mbalimbali unaendeshwa kwa misingi ya haki, uhuru na uwazi.
Imesisitizwa pia kuimarisha Misheni ya Uangalizi ya Uchaguzi ya SADC ili kusaidia kulinda misingi ya demokrasia.
Viongozi wa SADC walihimiza kuondolewa kwa vikwazo vinavyokwamisha muingiliano wa watu na biashara baina ya nchi wanachama, ikiwemo masharti ya viza na vikwazo visivyo vya kiforodha. Lengo ni kuimarisha mtangamano na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika ukanda huo.

You Might Also Like

Miradi Ufungaji Mifumo Ya Umeme Jua 20,000 Mbioni Kuanza

Kamati Ya Bunge Yapongeza Usimikaji Mfumo Wa Kidijitali CMA

Waziri Mkuu Aagiza Kuimarisha Ufuatiliaji Na Tathmini Kuleta Maendeleo

Ongezeni Uwajibikaji,Nidhamu, Utendaji Kazi – Bashungwa

Majaliwa Aituza UDSM kwa Kuongoza Eneo La Elimu, Utafiti, Ubunifu Sabasaba 2025

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Vyama Vya Wafanyakazi Himizeni Na Kufundisha  Amani Ya Nchi Kuelekea Uchaguzi Mkuu -Ridhiwan
Next Article REA Kusambaza Majiko Banifu 10,650 Mkoa Wa Pwani
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Majaliwa Apongeza Jeshi La Magereza Kurasimisha Ujuzi Kwa Wafungwa
Habari August 27, 2025
Mapokezi Ya Katibu Mkuu CCM  Dkt Migiro CCM, Aahidi Ushirikiano
Habari August 27, 2025
Majaliwa Aagiza Kuimarishwa kwa Mafunzo ya Ufundi Stadi Nchini
Habari August 27, 2025
VETA Yaanzisha Kozi Mpya ya Teknolojia ya Mifumo ya Viwandani
Habari August 26, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?