MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TAMWA Yawawezesha Wanawake Kupitia Mradi wa Nyuki
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TAMWA Yawawezesha Wanawake Kupitia Mradi wa Nyuki
Habari

TAMWA Yawawezesha Wanawake Kupitia Mradi wa Nyuki

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimetoa mafunzo ya ufugaji wa nyuki kwa wanawake wa kijiji cha Misufini, wilayani Kibaha mkoani Pwani, ili kuwawezesha kiuchumi na kuchochea uhifadhi wa mazingira kupitia uzalishaji na usindikaji wa mazao ya nyuki.
Akizungumza wakati wa mafunzo maalum kwa waandishi wa habari, Mkurugenzi wa TAMWA, Rose Reuben, amesema hatua hiyo ni sehemu ya mpango wa kuanzisha mradi wa mfano wa ufugaji wa nyuki katika shamba la shirika hilo lililopo Misufini.
“Shamba letu liko Misufini na tunataka majirani zetu hasa wanawake wanufaike na mradi huu. Lengo ni kuwawezesha kiuchumi kupitia shughuli endelevu,” amesema
Amesema nyuki ni chanzo muhimu cha kipato kwa kutumia rasilimali zilizopo kwenye mazingira ya asili, huku akieleza kuwa asilimia 80 ya shughuli za kilimo nchini hufanywa na wanawake.
“Kupitia ufugaji wa nyuki, wanawake watapata fursa ya kujipatia kipato endelevu kutoka kwa mazao kama asali, masega, chavua na gundi,” alieleza.
Kwa hatua ya awali, TAMWA inatarajia kuweka mizinga 200 ya nyuki kwenye shamba hilo kama sehemu ya utekelezaji wa mradi.
Naye Ofisa Biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Christina Samweli, amesema nyuki wana mchango mkubwa katika maisha ya binadamu, si kwa asali pekee bali pia kwa mazao mengine yenye thamani kubwa kiafya na kibiashara.
“Mazao ya nyuki kama chavua na gundi ni tiba na chakula. Lakini bado jamii nyingi hazijafahamu fursa hizi,” amesema.
Amesema wanawake kuchangamkia mafunzo hayo kwa kuwa yanatoa maarifa muhimu ya kutumia ardhi kwa tija bila kuharibu mazingira.
Aidha, ufugaji wa nyuki umetajwa kuwa ni shughuli rafiki kwa mazingira kwani hauhitaji ukataji wa miti wala matumizi ya kemikali, bali huchochea uhifadhi wa misitu na mimea.
Kupitia mradi huo wanawake wa Misufini wanatarajiwa kuwa mfano wa kuigwa katika matumizi bora ya rasilimali asilia kwa ajili ya maendeleo ya jamii na uhifadhi wa mazingira kwa vizazi vijavyo.
–

You Might Also Like

Ajali Yakatisha Maisha Ya Mkurugenzi  Mkuu Mtendaji TANESCO, Dereva Wake 

TFRA yazindua Chama cha wafanyabiashara wa Mbolea

Kanisa lakabidhi jengo la watoto la milioni 595 kwa serikali

Rais Samia atoa zaidi ya bil. 2.1 usimikaji wa mifumo, uendeshaji mashauri ya wafanyakazi

CCCC Yakutana na Wanahabari, Yapanga Mikakati Mipya 2025

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Nishati Safi Kwa Kila Mtanzania Inawezekana – Saidy
Next Article TARI Kibaha Yaboresha Pia Mbegu za Mazao ya Mizizi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Dodoma Yang’ara Katika Mfumo wa Stakabadhi Ghalani
Habari August 8, 2025
Samia, Nchimbi Kuchukua Fomu Ya Urais Kesho
Habari August 8, 2025
Mgombea Udiwani Manyoni Adhalilishwa, Rushwa Yadaiwa Kuvuruga Kura Za Maoni
Habari August 8, 2025
TOSCI: Mbegu Bora Ni Ajira, Biashara
Habari August 8, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?