MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Balozi wa Tanzania Nchini Italy Afurahishwa  Ubunifu wa TPHPA Maonesho ya Nanenane
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Balozi wa Tanzania Nchini Italy Afurahishwa  Ubunifu wa TPHPA Maonesho ya Nanenane
Habari

Balozi wa Tanzania Nchini Italy Afurahishwa  Ubunifu wa TPHPA Maonesho ya Nanenane

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read

Na Lucy Ngowi, Dodoma

DODOMA: BALOZI wa Tanzania nchini Italy, Mbarouk Nassor Mbarouk, ametembelea banda la Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma, na kuonesha kufurahishwa na ubunifu na kazi zinazofanywa na mamlaka hiyo.

Katika ziara hiyo, Balozi Mbarouk amesema amepata “exposure nzuri” juu ya majukumu na shughuli muhimu zinazotekelezwa na TPHPA, hasa katika kuhakikisha usalama wa mazao ya kilimo nchini na kutangaza bidhaa za wakulima wa Tanzania kwenye masoko ya kimataifa.

“Nimejifunza mengi kuhusu namna TPHPA inavyolinda afya ya mimea yetu, na pia kusaidia wakulima wetu kufungua masoko nje ya nchi. Hii ni kazi ya msingi katika maendeleo ya sekta ya kilimo,” amesema.

Awali, Meneja wa Sehemu ya Usimamizi wa Afya ya Mimea na Karantini, Musa Chidinda, alimueleza balozi kuwa hakuna mimea au mazao yabkilimo linaloruhusiwa kuingia nchini au kuuzwa sokoni bila kupitia hatua za uchunguzi, ukaguzi na kupewa vibali vya TPHPA.

“Mkulima yeyote anayetaka kuingiza au kuuza nje mazao yake lazima afuate taratibu za nchi. Tunadhibiti visumbufu vya mimea kuanzia shambani hadi kwenye mipaka yetu, kuhakikisha bidhaa zetu ni salama na zinakidhi viwango vya masoko ya kimataifa,” amesema Chidinda.

Katika mafanikio yanayoendelea kupatikana kupitia TPHPA, Chidinda ametaja kuwa mamlaka hiyo tayari imefanikiwa kufungua soko la parachichi, jambo ambalo limewapa fursa wakulima kuuza zao hilo nje ya nchi.

“Kwa sasa soko la parachichi limefunguliwa rasmi, na mchakato huu unahusisha ukaguzi wa zao hilo tangu lipo shambani hadi linapopelekwa sokoni. Tunahakikisha mkulima anapokea cheti ya usafi na mazao yake yanaingia sokoni kwa kufuata viwango vya ubora vilivyowekwa,” amesema..

Kwa ujumla, ushiriki wa TPHPA katika maonesho ya mwaka huu umeonesha wazi umuhimu wake katika kulinda afya ya mimea, kuzuia visumbufu vinavyoweza kuathiri kilimo, na kusaidia wakulima kufikia masoko mapya ya kimataifa.

You Might Also Like

Samia ashiriki mashindano ya dunia ya Quran

Wahitimu Kidato IV 2024, Washauriwa Kubadili Machaguo Ya Tahasusi

Umka yawashauri wakulima kutumia mbolea yake

Rais Samia afungua kikao kazi cha watendaji serikalini

CHAUMMA YAAPA KUJENGA BUNGE LA WABUNGE WA HOJA, SI MACHAWA

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Wadau Wakaribishwa Kuwekeza Katika Uchakataji, Biashara ya Mkonge Nchini
Next Article Bodi ya Maziwa Yatoa Mafunzo ya Ubora, Usalama wa Maziwa Katika Maonyesho ya Nane Nane
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?