MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TPHPA Yaleta Mapinduzi Mapya Katika Kilimo Kupitia Teknolojia ya Vinasaba
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TPHPA Yaleta Mapinduzi Mapya Katika Kilimo Kupitia Teknolojia ya Vinasaba
Habari

TPHPA Yaleta Mapinduzi Mapya Katika Kilimo Kupitia Teknolojia ya Vinasaba

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: MAMLAKA ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imezindua rasmi kifaa kipya cha kisasa aina ya MinION, chenye uwezo wa kutambua vinasaba vya wadudu, mimea, na magonjwa moja kwa moja shambani,
Teknolojia ambayo kwa mara ya kwanza upande wa kilimo inatumiwa Afrika na Tanzania ikiwa kinara.
Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA, Profesa Joseph Ndunguru amesema hayo katika maonesho ya Kilimo ya Nanenane Kitaifa na Kimataifa yanayofanyika mkoani Dodoma.
Amesema kifaa hicho ni mkombozi mkubwa kwa sekta ya kilimo nchini na kimethibitishwa kuwa na uwezo wa kutumika kwa mafanikio katika mazingira ya shamba.
Amesema kifaa hicho ambacho ni kidogo,  kinaweza kutoa majibu ya uchunguzi ndani ya dakika 20, kinatarajiwa kuleta mapinduzi katika sekta ya kilimo kwa kusaidia wakulima kupata majibu ya haraka kuhusu visumbufu vya mimea, hivyo kuwezesha matumizi sahihi ya viuatilifu na kuongeza tija ya uzalishaji.
“Kifaa hiki kilibuniwa Uingereza kwa ajili ya kutambua virusi vya Zika na Ebola, lakini sisi Tanzania tumefanya majaribio ya kina na tumethibitisha asilimia 100 uwezo wake katika kubaini visumbufu vya mimea, wadudu na magonjwa.
“Sasa kinatumiwa kwa mara ya kwanza Afrika hapa nchini kwetu,” amesema.
Amesema kupitia ushirikiano kati ya Umoja wa Ulaya (EU), Shirika la Chakula Duniani (FAO), na Serikali ya Tanzania, TPHPA imefanikiwa kupata vifaa 20 vya MinION ambavyo vitasambazwa kwenye vituo vya mamlaka hiyo katika kanda mbalimbali nchini.
Amesema lengo ni kuwezesha uchunguzi wa kisayansi wa wadudu, magonjwa na mimea sugu kwa haraka, katika maeneo yote ya Tanzania.
Ndunguru amebainisha kuwa teknolojia hiyo pia itasaidia kuongeza ushindani wa mazao ya Tanzania kwenye soko la kimataifa kwa kuwa sasa nchi itakuwa na uwezo wa kuthibitisha ubora wa mazao kwa haraka, kabla ya kuuza nje ya nchi.
“Hili ni jicho la kisayansi ambalo litazuia uingizwaji wa bidhaa zilizo na magonjwa hatari, na pia kusaidia kwenye utambuzi wa mimea, viumbe wa majini, wanyamapori na hata magonjwa ya binadamu,” amesema.
Naye Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Afya ya Mimea kutoka TPHPA, Dkt. Begnius Ngowi, amesema kifaa hicho kitaondoa ucheleweshaji wa majibu ya maabara na kukomesha utumiaji wa viuatilifu kwa kubahatisha.
“Changamoto kubwa imekuwa wakulima kutambua aina ya mdudu au ugonjwa kwa macho tu, na matokeo yake wanatumia dawa isiyofaa.
“Kwa mfano, mdudu Tuta absoluta maarufu kwa jina la ‘Kantangaze’ huonekana kama mdudu mwingine wa kawaida, lakini dawa zake ni tofauti kabisa,” amesema.
Amesema kupitia kifaa hicho, wataalamu wataweza kufanya uchunguzi wa kitaalamu hapo hapo shambani na kumpa mkulima suluhisho sahihi bila kuchelewa.
Baada ya maonesho hayo, wataalamu kutoka TPHPA wanatarajia kuanza kambi ya uchunguzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, mkoa wa Iringa, maarufu kwa kilimo cha mbogamboga na matunda, ili kubaini chanzo cha changamoto zinazowakabili wakulima wa eneo hilo.

You Might Also Like

Majaliwa Asisitiza Matumizi ya Mifumo ya Kieletroniki Katika Makusanyo

Biteko Amwakilisha Rais Samia Harambee Ujenzi Kanisa Katoliki

UDSM Chasaini Mikataba Na Kampuni Za Kichina, Kujengea Uzoefu Wanafunzi Wake

Serikali Yaongeza Bajeti Mfuko Wa Utamaduni Na Sanaa

OCPD Nguzo Kuu ya Utungaji Sheria – Dkt. Ndumbaro

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Tulia Atoa Taarifa Kifo Cha Ndugai
Next Article DC Atoa Wito kwa Tume ya Kurekebisha Sheria Kuzingatia Sheria Ndogondogo za Halmashauri
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mtego wa Inzi Wa Matunda Suluhisho Salama kwa Wakulima
Habari August 7, 2025
Mafua, Kifua Yadaiwa Kusababisha Kifo cha Job Ndugai
Habari August 7, 2025
Zimbabwe Yakabidhi Uenyekiti Kwa Madagascar
Habari August 7, 2025
Tume ya Kurekebisha Sheria Yatoa Onyo Kali kwa Wanaovunja Sheria za Umwagiliaji
Habari August 7, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?