MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: SADC Yatathmini Maendeleo ya Mpango wa RISDP Katika Mkutano wa 45 Madagascar
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > SADC Yatathmini Maendeleo ya Mpango wa RISDP Katika Mkutano wa 45 Madagascar
Habari

SADC Yatathmini Maendeleo ya Mpango wa RISDP Katika Mkutano wa 45 Madagascar

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
Antananarivo, Madagascar: MKUTANO wa 45 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umeanza rasmi leo, Agosti nne, 2025, jijini Antananarivo, Madagascar, kwa kuanza na Kikao cha Wataalamu cha Maofisa Waandamizi kinachojadili utekelezaji wa Mpango Mkakati Elekezi wa Maendeleo wa Kikanda wa mwaka 2030 (RISDP 2030).
Kikao hicho muhimu kimefunguliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Biashara za Kimataifa wa Zimbabwe, Balozi Albert Chimbindi, ambaye amesisitiza haja ya kufanya tathmini ya kina ya utekelezaji wa RISDP, sambamba na kubaini vikwazo vinavyokwamisha maendeleo ya miradi ya pamoja ya kikanda.
“Licha ya mafanikio yanayoonekana katika utekelezaji wa RISDP, bado kuna changamoto zinazohitaji mshikamano wa pamoja baina ya nchi wanachama. Tunahitaji kuongeza kasi ya utekelezaji, hasa katika miradi ya miundombinu na biashara ya ndani ya ukanda,” amesema Balozi Chimbindi.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mtendaji wa SADC anayeshughulikia Ushirikiano wa Kikanda, Angeles N’Tumba, ametoa wito kwa nchi wanachama kubuni mbinu za kudumu za upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya RISDP.
 Amependekeza kujifunza kutoka kwa jumuiya nyingine kama ECOWAS, ambayo imefanikiwa kuanzisha mifumo endelevu ya kutafuta rasilimali za maendeleo.
Mkutano huu wa SADC unatarajiwa kutoa mwelekeo mpya wa kisera na kiutekelezaji wa malengo ya RISDP, huku ukisisitiza mshikamano wa kikanda kama nguzo kuu ya maendeleo endelevu ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Ujumbe wa Tanzania katika kikao hicho unaongozwa na Mkurugenzi wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Talha Waziri, ambaye pamoja na wajumbe wengine wa nchi wanachama, wanashiriki katika mapitio ya kina ya utekelezaji wa RISDP ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi unaotarajiwa kufanyika Agosti 17, 2025.

You Might Also Like

SUA Yawafikia Wafugaji Wa Ng’ombe Wa Maziwa Kwa Tiba Mbadala Ya Homa Ya Kiwele

Benjamini Mkapa Yapandikiza Mimba 21, Watano Waongezewa Nguvu Za Kiume

NFRA Yawaalika Wadau Kununua Nafaka kwa Masoko ya Ndani na Nje

Zimbabwe Yakabidhi Uenyekiti Kwa Madagascar

Rais CWT Asikitishwa Na Uzembe, Maofisa Wa Halmashauri

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TARI Yaja Na Jawabu 88 Juu Ya Tindikali, Chumvi Kwenye Udongo
Next Article TARI Mlingano Yaleta Mapinduzi ya Mkonge, Viungo na Sayansi ya Udongo Tanzania
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?