MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Dkt Yonaz Awaasa Watumishi Ofisi Ya Waziri Mkuu  Kuongeza Bidii Katika Kutekeleza Majukumu Yao
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Dkt Yonaz Awaasa Watumishi Ofisi Ya Waziri Mkuu  Kuongeza Bidii Katika Kutekeleza Majukumu Yao
Habari

Dkt Yonaz Awaasa Watumishi Ofisi Ya Waziri Mkuu  Kuongeza Bidii Katika Kutekeleza Majukumu Yao

Author
By Author
Share
2 Min Read

Na Mwandishi Wetu

KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amewaasa Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Ameyasema hayo wakati akifungua mkutano na Watumishi wa Ofisi hiyo na kusema ni  muhimu kuwa na nidhamu ya kazi, kushirikiana na kuendelea kuwa wabunifu katika majukumu ya kila siku, na kuwakumbusha watumishi kuwa kazi wanazofanya zinagusa maisha ya mamilioni ya wananchi, hivyo ni wajibu wa kila mtumishi kuhakikisha anatoa huduma bora na kwa viwango vya juu.

“Pia, nawasihi kuendelea kujenga mshikamano miongoni mwenu. Tunaposhirikiana, tunajenga nguvu ya pamoja ambayo hakuna changamoto inayoweza kutuzuia. Nawaomba tuendelee kufanya kazi kwa bidii na kwa moyo mmoja. Kumbukeni kuwa, kila mchango wenu una thamani kubwa katika kufanikisha malengo ya Ofisi yetu na Taifa kwa ujumla.” Amefafanua Dkt. Yonazi.

Katibu Mkuu Yonazi aliendelea kusema kuwa, katika kuboresha Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Ofisi imeendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa kushughulikia changamoto zinazohusu mazingira ya kazi na maslahi ya wafanyakazi ikiwa ni pamoja na  kukuza ubunifu katika utendaji kazi wa kila siku na kuimarisha mifumo bora zaidi ya kufuatilia maendeleo ya kazi na kuhakikisha kila mfanyakazi anawajibika ipasavyo kwa nafasi yake.

Katika mkutano huo watumishi wataweza kupata elimu kutoka kwa wataalam wa  Mfuko wa Uwekezaji wa UTT kuhusu umuhimu wa kuwekeza, pamoja na mambo mengine pia watapewa elimu  itakayowakumbusha masuala mbalimbali yanayohusu uzingatiaji wa maadili ya utumishi wa umma, masuala ya Afya hususan homa ya ini na magonjwa yasiyoambukizwa.

 

 

 

 

You Might Also Like

Waajiri Wathamini Taaluma Ya Uandishi Wa Habari – Dkt. Mkoko

TASAC yajipanga kuhudumia wafanyabiashara

Wazazi washauriwa kusomesha watoto useremala

Majaliwa Ataka Yatolewe Mafunzo Yanayozingatia Soko La Ajira

DART Toeni Fursa Kwa Watanzania Kuwekeza kwenye Mwendokasi -Mchengerwa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Wagombea Wa CCM Dodoma Mjini Waanza Kujinadi kwa Wajumbe
Next Article Ajira kwa Vijana na Afya kwa Wazee: Ajenda Kuu za Wagombea Jimbo la Dodoma Mjini
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Malecela: Nitakuza Vipaji, Nitafutia Vijana Ajira Dodoma Mjini
Habari July 31, 2025
Njaa, Mafao Ya Wakulima Vyatikisa Kampeni Za Ubunge Dodoma Mjini
Habari July 31, 2025
Asha Moto Aibuka Kidedea Ubunge wa Viti Maalum Mtwara Kupitia CCM
Habari July 31, 2025
TUCASA Yatoa Mapendekezo ya Sheria, Sera Kwa Serikali Kutatua Ucheleweshaji Wa Malipo
Habari July 31, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?