MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Majaliwa Aomba Watanzania Wapatiwe Mafunzo Belarus Kuendeleza Kilimo
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Majaliwa Aomba Watanzania Wapatiwe Mafunzo Belarus Kuendeleza Kilimo
Habari

Majaliwa Aomba Watanzania Wapatiwe Mafunzo Belarus Kuendeleza Kilimo

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Mwandishi Wetu
BELARUS: WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, ameomba Watanzania wapewe fursa za mafunzo katika Chuo cha Kilimo cha Belarus ili kujenga uwezo wa kitaalamu utakaosaidia kuleta mapinduzi katika sekta ya kilimo nchini.
Akizungumza mara baada ya kutembelea chuo hicho akiwa kwenye ziara rasmi ya siku mbili nchini Belarus, Majaliwa amesema elimu ya kilimo kwa vitendo inayotolewa chuoni hapo ni fursa adhimu kwa Watanzania kupata maarifa ya kisasa yatakayosaidia kuongeza tija na usalama wa chakula nchini.
“Watanzania wakipata elimu bora ya kilimo, wakirudi wataibadilisha nchi yao. Tutaleta mapinduzi ya kijani kwa kutumia teknolojia na ujuzi mpya,” amesema.
Waziri Mkuu amehimiza kuanzishwa kwa ushirikiano kati ya chuo hicho na taasisi za elimu za ndani, huku akiahidi kuwa Serikali ya Tanzania iko tayari kuwezesha utekelezaji wa mpango huo.
Mbali na elimu,Majaliwa pia alitembelea viwanda vya kutengeneza matrekta na zana za kisasa za kilimo na kuhamasisha wawekezaji hao kufungua matawi yao nchini Tanzania.
Amesema uwepo wa viwanda hivyo nchini utapunguza gharama kwa wakulima na kuongeza upatikanaji wa zana bora za kilimo.
Katika siku zake mbili nchini Belarus Julai 2 hadi 23, 2025, Waziri Mkuu ametembelea kampuni nane kubwa za mitaji mjini Minsk na kunadi fursa za uwekezaji nchini Tanzania katika sekta kuu nne za kipaumbele: kilimo, afya, madini na ulinzi na usalama.
Kwenye sekta ya Afya, Waziri Mkuu ametembelea kampuni ya Belmedpreparaty, moja ya wazalishaji wakubwa wa dawa na vifaa tiba nchini Belarus, inayozalisha bidhaa zaidi ya 1,700 zinazouzwa ndani na nje ya nchi.
Ametoa wito kwa kampuni hiyo kuwekeza nchini Tanzania kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa dawa zenye ubora na bei nafuu.
Hivyo Kampuni hiyo imekubali kutuma ujumbe wake Tanzania kwa ziara ya tathmini ya uwekezaji.
Akizungumzia sekta ya madini baada ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza mitambo ya kuchimba migodini, amewahamasisha wawekezaji hao kuja kuwekeza nchini ili kuongeza ufanisi wa uchimbaji na kuchochea ukuaji wa sekta hiyo muhimu.
Pia  Majaliwa ametembelea kiwanda cha vifaa vya uokoaji na zima moto na kusisitiza umuhimu wa kushirikiana na kiwanda hicho ili kuondoa changamoto ya uhaba wa vifaa vya maokozi nchini Tanzania.
Ziara ya Waziri Mkuu nchini Belarus ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na kuvutia uwekezaji wa kimkakati kwa maendeleo ya Taifa.

You Might Also Like

Tanzania Ina Utolevu Wa Chakula Kwa Miaka Minne Uongozi Wa Samia

Twendeni Tukapige Kura Ya Ukombozi, CHAUMMA Yahitimisha Kampeni

Wanafunzi 431, Watumishi 52 Watembelea TARI kujifunza Kilimo

Samia Mgeni Rasmi Siku Ya Wanawake Jijini Arusha

Serikali Yapeleka Sh Bil 10 Kwa Kiwanda Cha Viuadudu Cha TBPL

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Benki Ya Dunia Kujenga Mradi Wa Njia Ya Kusafirisha Umeme Wa KV 400  Kutoka Uganda-Tanzania  
Next Article Mkenda Atoa Tuzo kwa Waajiri Wanaowasilisha Michango kwa Wakati
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

CAG Aipongeza TARURA Kwa Ujenzi Wa Miundombinu
Habari January 9, 2026
Tuna Deni La Kusimamia Miradi Na Kusikiliza Kero za wananchi Ili Kuleta Maendeleo Ya Kweli-Salome
Habari January 9, 2026
Rais Dkt Samia Azindua Majengo Ya Kisasa
Habari January 8, 2026
TEA, UNICEF Watekeleza Miradi ya Elimu Visawani Zanzibar
Habari January 8, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?