MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Tanzania, Uturuki Zaweka Dira Mpya ya Biashara ya Dola Bil. Moja
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Tanzania, Uturuki Zaweka Dira Mpya ya Biashara ya Dola Bil. Moja
Habari

Tanzania, Uturuki Zaweka Dira Mpya ya Biashara ya Dola Bil. Moja

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM: TANZANIA imeweka malengo makubwa ya kupanua ushirikiano wake wa kiuchumi na Uturuki kwa kufikia biashara ya thamani ya Dola za Kimarekani Bilioni moja, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kukuza uchumi kupitia diplomasia ya biashara.
Akizungumza  Mkoani Dar es Salaam wakati wa kusainiwa kwa Azimio la Kamati ya Pamoja ya Biashara (JTC) kati ya Tanzania na Uturuki, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo, amesema  hatua hiyo inalenga kuongeza thamani ya bidhaa za Tanzania zinazopelekwa kwenye soko la Uturuki.
“Kupitia timu ya wataalamu na ushirikiano wa sekta binafsi, tutaweka msingi imara wa kukuza mauzo yetu na kuifanya biashara kuwa lango kuu la fursa kwa wananchi wetu,” amesema Dkt. Jafo.
Dkt. Jafo amesema kuna fursa kubwa ambazo bado hazijatumika kikamilifu katika sekta za viwanda, kilimo, na madini, huku akisisitiza kuwa Tanzania inajifunza teknolojia ya kisasa kutoka kwa washirika wao wa Uturuki ili kuongeza ufanisi wa uzalishaji wa ndani.
“Teknolojia ya Uturuki kwenye viwanda na kilimo ni ya kiwango cha juu. Ushirikiano huu utatufungulia milango ya maarifa na kuongeza tija kwa Watanzania,” amesema.
Uhusiano kati ya Tanzania na Uturuki umeimarika kwa kasi katika muongo uliopita, hasa kufuatia kufunguliwa kwa balozi za nchi hizo mwaka 2009 na 2017 mtawalia. Ziara za viongozi wakuu — akiwemo Rais Recep Tayyip Erdoğan na Rais Samia Suluhu Hassan — zimechochea zaidi mashirikiano hayo.
Kwa upande wake, Kaimu Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Ali Goktug IPEK, amesema kuwa JTC itakuwa chombo muhimu cha kuondoa vikwazo vya kibiashara na kurahisisha uwekezaji kati ya pande hizo mbili.
“Tutaendelea kushirikiana kwa karibu katika maeneo ya miundombinu, kilimo, nishati na teknolojia. Kamati hii itakuwa jukwaa la maendeleo ya pamoja,” amesema IPEK.
Amehitimisha kwa kusema kuwa chini ya uongozi wa Rais Erdoğan na Rais Samia, nchi hizo mbili zitajenga uhusiano wa kiuchumi wenye misingi ya uadilifu, maendeleo na ustawi wa pamoja.

You Might Also Like

Polisi Dodoma Yawataka Wananchi Kutoa Taarifa 

TPHPA ina mchango mkubwa utoshelevu wa chakula – Profesa Ndunguru

Usajili Kwa Njia Ya Mtandao, Umeharakisha Ufunguaji Mashauri

Bajeti ya TUGHE 2025 Yaidhinishwa

Miradi iliyokamilika ianze kutoa huduma- Nyamoga

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TUICO Arusha Yapongezwa Na AUWSA
Next Article Maliasili Yapongezwa Kwa Kutekeleza Maono Ya Rais Samia  
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Kichina Chatamba UDSM: Walimu Watanzania, Wachina Wapewa Tuzo kwa Umahiri
Habari July 25, 2025
Samia Mgeni Rasmi Siku Ya Mashujaa
Habari July 24, 2025
Mkenda Atoa Tuzo kwa Waajiri Wanaowasilisha Michango kwa Wakati
Habari July 24, 2025
Majaliwa Aomba Watanzania Wapatiwe Mafunzo Belarus Kuendeleza Kilimo
Habari July 24, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?