MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: NFRA Yawaalika Wadau Kununua Nafaka kwa Masoko ya Ndani na Nje
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > NFRA Yawaalika Wadau Kununua Nafaka kwa Masoko ya Ndani na Nje
Habari

NFRA Yawaalika Wadau Kununua Nafaka kwa Masoko ya Ndani na Nje

Author
By Author
Share
2 Min Read

Na Lucy Ngowi

DAR ES SALAAM: WAKALA wa Taifa wa Uhifadhi wa Chakula (NFRA) umefungua milango kwa wadau mbalimbali kushiriki katika biashara ya nafaka, kwa kuwataka wafanyabiashara, wakulima na wananchi kununua nafaka zilizohifadhiwa kwa ubora ili ziuzwe katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

Akizungumza kwenye Maonyesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara yajulikanayo kama Sabasaba, Ofisa Masoko wa NFRA, Eva Michael amesema wakala upo kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu uhifadhi wa chakula,

Ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wafanyabiashara na wakulima kushiriki kikamilifu kwenye mnyororo wa thamani wa uhifadhi wa chakula nchini.

“Tupo hapa kutoa elimu ya uhifadhi wa chakula, lakini pia kuwakaribisha wadau wote wanaotaka kushiriki kwenye biashara ya nafaka. Kwa sasa tunaendelea na maandalizi ya awali ya msimu wa ununuzi wa nafaka mpya, lakini pia tunaendelea na mauzo ya nafaka zilizopo,” amesema.

Amesema NFRA ina akiba ya kutosha ya nafaka katika maghala yake, ikiwa ni pamoja na mahindi, mpunga, mtama mweupe, mbaazi na dengu, huku akisisitiza kuwa chakula hicho ni salama na kimetunzwa kwa viwango vya kitaalamu.

Amebainisha kuwa fursa hiyo ni muhimu kwa wafanyabiashara wanaotaka kupata nafaka kwa bei nafuu na kuuza kwenye masoko mbalimbali, hatua inayolenga pia kuimarisha usalama wa chakula na kuchochea uchumi wa taifa kupitia sekta ya kilimo na biashara.

Wakala wa NFRA ni taasisi ya serikali inayoshughulika na uhifadhi wa chakula cha dharura kwa ajili ya kukabiliana na majanga ya njaa, lakini pia imekuwa mshirika muhimu wa sekta binafsi kupitia usambazaji wa nafaka kwa ajili ya biashara.

You Might Also Like

Mkenda Atoa Tuzo kwa Waajiri Wanaowasilisha Michango kwa Wakati

TPHPA yaonyesha ufanisi mkubwa udhibiti wa panya, kwelea kwelea

Mdemu Azindua Utafiti Uliofanywa na FES Kwa Kushirikiana Na COTWU – T

Hospitali ya Temeke kufanyiwa maboresho eneo la huduma Kwa wateja

RC Dodoma Atoa Maagizo Kwa Ma – DC Kuhusu Ukame

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Kafulila: Ushirikiano wa Sekta Binafsi na Umma Kuboresha Huduma
Next Article Nyanya Cheri na Ngogwe Chungu Zarejea 
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Majaliwa Apongeza Jeshi La Magereza Kurasimisha Ujuzi Kwa Wafungwa
Habari August 27, 2025
Mapokezi Ya Katibu Mkuu CCM  Dkt Migiro CCM, Aahidi Ushirikiano
Habari August 27, 2025
Majaliwa Aagiza Kuimarishwa kwa Mafunzo ya Ufundi Stadi Nchini
Habari August 27, 2025
VETA Yaanzisha Kozi Mpya ya Teknolojia ya Mifumo ya Viwandani
Habari August 26, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?