Na Lucy Lyatuu
CHuo Kikuu Cha Dar es Salaam )UDSM),TaasisiI ya Teknolojia imemaliza Kufanya Utafiti Wa dawa maalum ya kusafisha sumu kwenye maji na imebaini Ina Uwezo Wa Kuondoa sumu kwenye maji kwa asilimia 93.5.
Mhadhiri Msaidizi kutoka Taasis Ya Teknolojia UDSM Veronica Siwalima amesema hayo katika Banda la UDSM lililoko katika maoneshobya 49 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayonyika Dar es Salaam.
Amesema chini ya Mradi huo Wa kutafita dawa ya kusafisha maji unaojulikama kama BC5 umetafiti maji ya bahari ya Hindi kuanzia Pemba,Unguja,Dar es Salaam, na Mtwara kujua sumu zilizopo kwenye maji.
“Tumefanya Utafiti kuangalia sumu kwenye maji haswa kwenye miji mkubwa kama Dar es Salaam na Zanzibar iwapo imechafuliwa na sumu nzito na kutafita ufumbuzi Wa Kuondoa hizo sumu,” amesema na kuongeza kuwa Kuna bidhaa inaaitwa Carbonnone tubes ambazo ni malighafi za Kisasa zinazotumika Kuondoa sumu kwenye maji.
Amesema malighafi hizo zimetengenezwa viwandani haswa kwa nchi zilizoendelea na mbadala WA hizo unaweza kutumia chupa maalum za plastiki zinazoitwa polypolyn plastiki.
Amesema chupa hizo zinatumika kwa kuzichoma kutengeneza gesi ambayo ndio inaondoa sumu kwenye maji na ilipotafitiwa ikabainika Kuondoa sumu kwenye maji kwa asilimia 93.5.
“Pia tumechukua maji kutoka viwandani na maji ya mto Kizinga ambayo tumekuta yamechafuliwa na sumu na dawa hiyo ikaweza Kuondoa sumu kwa asilimia 92”,amesema na kuongeza kuwa hivyo matarajio Yao yamefanikiwa ya namna ya Kuondoa sumu kwenye maji .
Amesema Kwa sasa wamemaliza kuangalia kuhusu hayoaji yalivyochafiliwa na wanatafita ithibati kwa ajili ya kukubalika na kutumia kwenye viwanda Ili kutumia kusafishaaji Yao kabla ya kuyatiririsha..
Veronica amesema sumu hizo zilizoko kwenye maji ikiwemo Yale yanayotiririshwa kutoka viwandani hutumia kumwagiliaboga za majani,baharini kwenye samaki hivyo hurudi kwa binadamu kutokana na matumizi.
“Hivyo kupitia Utafiti huo ni Waziri kuwa dawa hiyo Inawezesha kuwa suluhisho kwa wenye viwanda vinavyottitisha maji na hata baharini tukawa salama,” amesema na kuongeza kuwa athari zitokanazo na sumu hizo haswa sumu aina ya led ikiingia kwa binadamu husababisha saratani.
Ameishauri serikali kuboreshaa ma abara za vyuo vikuu ziwe na Vifaa vyote Ili zirahisishe Kufanya tafiti kubwa na ndogo.