Na Lucy Lyatuu
MAMLAKA Ya Kudhibiti Mkondo Wa Juu Wa Peteoli (PURA) inajivunia agenda ya Nishati Safi ya kupikia iliyoanzishwa na Rais Samia Suluhu Hassan na kwamba wanaitekeleza kwa vitendo.
Imesema katika maonesho ya biashara ya Kimataifa maarufu kama sabasaba imeona mwamko umekuwa mkubwa Wa suala la Nishati Safi na kwamba watendaji wamekuwa wakiitekeleza kwa vitendo bila kumuangusha Rais Samia.
Mkurugenzi Mkuu wa PURA Charles Sangweni amesema hayo katika banda la PURA lililoko kwenye maonesho ya biashara ya Kimataifa maarufu kama sabasaba na kuongeza kuwa kazi ya Mamlaka hiyo ni udhibiti wa shughuli zote za utafutaji,uzalishaji na uendelezaji Wa shughuli za mafuta na gesi
Amesema PURA imekuwa ikishirikinkatika maonesho hayo kuanzia 2017 na kwamba Kila mwaka kumekuwa na maboresho Makubwa wamekuwa wakiyaona na kwa mwaka 2025 mambo yamekuwa mazuri zaidi.
“Kwa mwaka huu katika maonesho haya vitu vingi vimeenda kidijitali zaidi lakini mwamko Wa wananchi umekuwa mkubwa na idadi ya wanaoingiankatika Banda letu imekuwa kubwa kuliko miaka yote,” amesema.
Amesema na maswali yanayoulizwa Yana maana jambo linaloonesha jinsi Wananchi walivyojenga uelewa mkubwa wa mafuta na gesi.
Kuhusu PURA amesema wakati Mamlaka inaanzishwa ushiriki Wa watanzania hasa kwenye ajira na kampuni za utafitaji,Uzalishaji Uendelezaji shughuli za Mafuta na Gesi ilikuwa chini ya asilimia 55 lakini kwa sasa ni asilimia 85.
Amesema kuongezeka kwa kiwango hicho kunapimwa kwa kukusanya data na kwamba walizoea Kuna meli ikija kwa ajili ya utafitaji Mafuta ikiwa na watumishi wa nje lakini kwa sasa hata Wa ndani ya nchi wanaonekana.
“Watanzania wamepata uzoefu kutoka kwa watu na katika kushiriki miradi iliyofanywa huko nyuma,” amesema na kuongeza kuwa PURA Ina mirafi mbalimbali inayotekeleza na kwamba kwa sasa wako kwenye maandalizi ya kuchimba visima vitatu Mtwara na kwenye vitalu ushiriki Wa Watanzania uko kwa asilimia 40.
Amesema pamoja na ushiriki huo kukua lakini Mamlaka itahakikisha kazi zote zinafanywa na watanzania na katika kampuni 10 za utafutaji sita kati ya hizo ni za Watanzania.
“Na nafasi za uongozi karibu asilimia 95 ni za Watanzania kwani Mamlaka imejitahidi maeneo yote kuweka watanzania” amesema huku akiipongeza serikali.
MWISHOOOOajivunia Agenda Ya Matumizi Ya Nishati Safi