Na Lucy Lyatuu
NAIBU Waziri wa Katiba na Sheria Jumanne Sagini amesema Wizara hiyo inatoa kipaumbele elimu kwa umma hususani katika masuala yanayolalamikiwa kuhusu umiliki wanardhi.
Amesema hayo alipotembelea Banda la Wizara hiyo lililoko katika maoneshobya 49 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama sabasaba yanayoendelea Dar es Salaam.
Amesema huduma ya msaada wa kisheria inahitajika kwa watanzania wali wengi hivyo Wizara hiyo inalifanya kazi ya kutoa huduma ya msaada wa kisheria kuwa endelevu.
Amesema maofisa na wasajili wa ardhi waliopo ngazi ya Mkoa wanatakiwa kuwaelimish wananchi juu ya utaratibu wa kumiliki ardhi hata hati ya kumiliki hati ya ardhi,
Sagini amesema wananchi wakipatiwa elimu ya ardhi malalamiko hayatakuwa mengi huku akiishukuru serikali ya RAIS Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na uboreshaji mkubwa wa nyanja mbalimbali.
“Pia kwa mabanda ambayo yanaigusa sekta ya Katiba Sheria na utoaji wa haki, tukianzia mahakama katika maonesho haya inaonekana walivyojipanga,Idara zote za mahakama zipo kwa ajili ya utoaji wa elimu na masuala mbalimbali yanayohusu mahakama,” amesema na kuwataka wananchi kutumia maonesho hayo Kupata elimu.
Amesema banda la Wizara ya Katiba na Sheria limesheheni ubora ambapo limepata zawadi kwa kuwa mshindi wa jumla namba moja katika maonesho .
Kuhusu Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA),amesema alitembelea banda la wakala huo na kuona namna huduma inavyotolewa na kwamba alibaini watu wengi wamejitokeza kwa ajili ya kuomba vyeti vya kuzaliwa.
Hata hivyo amesema lipo pengo kuhusu taarifa kwamba wananchi wanakosa kufahamu huduma za utoaji wa vyeti vya kuzaliwa zipo hadi ngazi za Wilaya.
Amesema hakuna sababu yoyote wananchi kusubiri Saba Saba ndo waje wabanane katika ufuatiliaji wa utoaji wa vyeti hivyo huku akisema wakifika Saba Saba wanakuta vyeti vimeshapelekwa Wilaya ambapo wananchi hao wanatoka