Na Lucy Lyatuu
MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) imewashauri wajasiriamali
wanajishughilisha na shughuli za kemikali bila usajili
kutembelea maonesho ya Biashara ya Kimaraifa maarufu kama Sabasaba Ili kupewa maelekezo ya taratibu zakufuata ili kukamilisha usajili.
Akizungumza katika viwanja vya maonesho ya Sabasaba Mkurugenzi wa Huduma za Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira Dk.Peter Shimo amesema mamlaka hiyo ipo katika maonesho hayo kwa ajili yakuendelea kutoa elimu ya masuala mbalimbali hasa ya katika masuala ya kemikali.
Amesema inawataka wajasiriamali wanaojishughulisha na kemikali kufika katika Maonesho ili kuweza kupata elimu kuhusu kemikali pamoja na kufanya usajili wa bidhaa hiyo

Amesema Huduma wanazozitoa ni pamoja na usajili wa kemikali kwa maana kwamba ,wahusika wanaofika katika Banda hilo wanapata elimu kuhusu shughuli zinazofanywa na Mamlaka hiyo lakini pia kuhusu usajili wa wajasiriamali wanaojihusisha na masuala ya kemikali.
Amesema mamlaka pia ina mfumo wa kusajili wajasiriamali mtandaoni kwa ajili ya watu ambao wapo mbali na watoa huduma hiyo.
“Ambao wapo mbali na ofisi zetu nao waje hapa kwenye banda ili wapate usajili kwa njia ya mtandao,”amesema.
Amesema lengo la GCLA ni kuhakikisha jamii inapata elimu ya kemikali na mambo mengine yanayohusiana na mamlaka katika maeneo yote.