MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Wanafunzi UDOM Wavumbua Mafuta ya Asili Kutoka Mabaki ya Zabibu
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Wanafunzi UDOM Wavumbua Mafuta ya Asili Kutoka Mabaki ya Zabibu
Habari

Wanafunzi UDOM Wavumbua Mafuta ya Asili Kutoka Mabaki ya Zabibu

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
Dar es Salaam;: WANAFUNZI kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wameibuka na uvumbuzi wa kipekee wa mafuta ya nywele na ngozi, wakitumia mabaki ya zabibu yaliyokuwa yakitupwa baada ya matumizi ya awali ya matunda hayo.
Hayo yamebainika katika  Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea mkoani Dar es Salaam, maarufu kama Sabasaba, ambapo wanafunzi hao ni miongoni mwa washiriki wakionesha bidhaa zao za ubunifu.
Akizungumza kwa niaba ya chuo hicho, Mwakilishi wa UDOM, Uswege Mwangoge amesema mradi huo ulianzishwa baada ya wanafunzi kubaini kuwa mabaki ya zabibu yanatupwa hovyo, hivyo kuchafua mazingir hali  iliwachochea kufikiri na kutafuta namna ya kuyatumia mabaki hayo kwa njia endelevu.
“Tuliona ni upotevu mkubwa kuacha mabaki haya yapotee bure au kuchafua mazingira. Tukafanya utafiti na kugundua kuwa yana virutubisho vingi muhimu kwa ngozi na nywele,” amesema Mwangoge.
Kwa mujibu wa Mwangoge, mafuta hayo yana sifa nyingi za kiafya, ikiwemo uwezo wa kupenya haraka kwenye ngozi, kulainisha, kulinda na kusaidia ngozi kurejea katika hali yake ya asili bila kutumia kemikali hatarishi.
“Mafuta haya yana vitamini nyingi, hayana kemikali, hayachomi ngozi wala kusababisha madhara. Yanasaidia kulainisha ngozi, kuimarisha vinyweleo na kutoa kinga ya asili dhidi ya uharibifu wa ngozi,” amesema.
Mradi huo ni sehemu ya juhudi za UDOM kuhimiza ubunifu, ujasiriamali na matumizi ya teknolojia bunifu kwa ajili ya maendeleo endelevu na kukuza uchumi wa viwanda kupitia tafiti za wanafunzi.
Kwa sasa, wanafunzi hao wapo katika hatua ya majaribio ya soko huku wakitafuta wadau na wawekezaji watakaosaidia kuongeza uzalishaji na kufikisha bidhaa hiyo sokoni kwa wingi.

You Might Also Like

Mpango Mkakati wa Takwimu wazinduliwa

Atoa Maelekezo Kwa Chuo Cha Hombolo Kuwajengea Uwezo Viongozi Wa Mitaa Na Vijiji -Kapinga

Waziri Mkuu Aagiza Kuimarisha Ufuatiliaji Na Tathmini Kuleta Maendeleo

TUCTA Yaanza Maandalizi Ya Mei Mosi

Mpogolo Aipongeza Halmashauri Maandalizi Mikopo Asilimia 10

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Taasisi Ya Confucius Imezindua Kitabu Cha Kujifunza
Next Article UDOM Yatafiti Dawa za Malaria, Vidonda vya Tumbo, Kisukari Kutoka Mimea ya Asili
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NBS: Utumiaji Wa Takwimu Nyenzo Muhimu Kwa Mama Lishe
Habari July 5, 2025
FCC Yatoa Elimu Ya Ushindani Wa Kibiashara Katika Maonesho Ya  Biashara
Habari July 5, 2025
Watanzania Watakiwa Kuachana Na Dhana Potofu Kuwa Nishati Safi Ya Kupikia Ni Gharama
Habari July 5, 2025
Wananchi Waelimishwe Kuhusu Utendaji wa Kamati za Maadili za Maofisa wa Mahakama
Habari July 5, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?