Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: CHUO Kikuu cha Dodoma (UDOM), kimefanya utafiti wa kubadili plastiki kupata mafuta mazito na mkaa.
Akizungumza katika maonesho ya Sabasaba mkoani Dar es Salaam, Mhadhiri wa chuo hicho, Dkt. Adrian Pamaini alieleza hayo kwa Mfanyakazi Tanzania.
Amesema kutokana na plastiki kusambaa ovyo wametatua changamoto hiyo kwa kutengeneza bidhaa hizo ambapo mafuta mazito yanatumika kwenye mitambo mbalimbali ya viwanda.
“UDOM tumekuja na jawabu la kuchukua plastiki kubadili kupata mafuta hayo mazito na mkaa.
” Tunachoma plastiki joto la juu na kupozwa ndipo yanapatikana mafuta hayo. Mabaki yake kutengenezea mkaa na tiles.
“Tunaendelea na utafiti zaidi. Na katika utafiti wetu tuliona ukichoma kilo moja ya plastiki inaweza kutoa mafuta nusu lita,” amesema.
Ameongeza kwamba utafiti huo utapunguza usambaaji ovyo wa plastiki mitaani.