Na Danson Kaijage
DODOMA: WAKILI Msomi Anthony Kanyama amechukua fomu ya kugombea nafasi ya ubunge katika Jimbo jipya la Mtumba jijini Dodoma.
Kanyama amechukua fomu hiyo akiwa wa pili, baada ya aliyekuwa mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde kuchukua fomu ya kuomba kugombea ubunge katika jimbo hilo.
Mara baada ya kukabidhiwa fomu ya kuomba ridhaa hiyo na Katibu wa CCM wilaya ya Dodoma Mjini, Sophia Kibaba, Kanyama amesema amefanya uamuzi huo kwa mujibu wa katiba ya chama na serikali.