MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TARURA Dar Yaendelea Na Ujenzi Wa Miundombinu Ya Barabara Iliyosimama Kutokana Na Mvua
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TARURA Dar Yaendelea Na Ujenzi Wa Miundombinu Ya Barabara Iliyosimama Kutokana Na Mvua
Habari

TARURA Dar Yaendelea Na Ujenzi Wa Miundombinu Ya Barabara Iliyosimama Kutokana Na Mvua

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Mwandishi Wetu

IMEELEZWA kwamba uwepo wa mvua nyingi  Dar es Salaam imesababisha ujenzi wa barabara katika maeneo yenye zabuni kusimama kufanya kazi katika kipindi cha miezi miwili.

Hayo yameelezwa na Meneja wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) mkoa wa Dar es Salaam,  Geofrey Mkinga wakati akikagua maeneo ambayo yapo chini ya wazabuni.

Amesema hayo wakati akikagua barabara ya Tabata-Mazda (mita 500), Tabata-Kinyerezi kuelekea Sokoni (kiwango cha zege) pamoja na barabara ya Kivule-Msongola (km 9) na barabara kuelekea hospitali ya wilaya na Majohe (Km. 2.7).

“Kama tulivyotoa taarifa mwanzo kwamba kazi nyingi zilikuwa zimesimama kutokana na uwepo wa mvua nyingi zilizonyesha hivyo kwasasa tumeshawaagiza wakandarasi warudi ‘site’ na kuanza kazi mara moja”.

“Wakati wa mvua nyingi wakandarasi hawakuweza kukusanya malighafi na hata kuingia kwenye machimbo, pia huwezi kuweka ‘material’ ya udongo kipindi hicho’ ameongeza kusema.

Hata hivyo,  amewataka wakandarasi wote waliopewa zabuni za ujenzi wa barabara katika mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha wanaingia kazini ili kazi walizopewa zikamilike kwa wakati.

 

 

Kwa barabara ya Msongola-Kivule,  Mkinga amemuagiza Mkandarasi kuendelea na kazi hiyo hadi Desemba mwaka huu awe ameshatoka hatua za awali na kubakiza kuweka tabaka la lami pamoja na mifereji.

“Kama unavyoona kuelekea hospitali ya wilaya na Majohe, ilikuwa barabara mbovu na wananchi wamekuwa wakilalamikia ila kwa sasa hamna kazi iliyosimama na maendeleo ya mradi ni mazuri.

Naye, Meneja wa Ilala  John Magori amesema wataendelea kuwabana wakandarasi kuhakikisha maeneo yote yenye mikataba yanafanyiwa kazi kwa wakati ili kusudi changamoto za barabara ziishe.

Amesema, wakandarasi katika kata zote wameshaanza kurudi ‘site’ na kazi zimeanza ikiwemo katikati ya jiji, Tabata, Kitunda na Upanga.

Mkazi wa Msongola,  Peter Marwa amemshukuru Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa barabara hizo kwani itawaondolea adha ya usafiri katika  Kata ya Msongola-Jimbo la Kivule.

Wakati huo huo,  Mkandarasi anayejenga barabara ya Segerea,  Lookman Msanguka amesema kazi zilisimama kwa kipindi fulani ila kwa sasa kazi zinaendelea na hivyo ameaahidi kufanya kazi na kukamilisha mradi huo kama ulivyopangwa.

“Changamoto zilikuwepo  kutokana na mvua kwani huwezi kufanya kazi ya zege na kushindilia vifusi kipindi cha mvua hivyo tulisimama kwa miezi miwili ila kwasasa tunapambana ili kwenda sawa na kilichokuwepo kwenye mikataba”.

You Might Also Like

Waziri Mkuu Majaliwa Amwakilisha Dkt.Mpango Mahafali Ya 43 OUT

Ufugaji wa sungura ni fursa  – UDOM

Nzega Kujenga Barabara za Lami, Soko la Kisasa ili Kukuza Uchumi

Hazina yaanza kuwalipa wanachama 465 wa TALGWU

SPIKA asisitiza matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Serikali Yazidi Kuhamasisha Nishati Safi, Yatoa Mitungi 225 Kwa Watumishi Gereza kuu Maweni
Next Article Mitambo 10 Ya Uchimbaji Madini Yenye Thamani Ya Bilioni 10 Yazinduliwa
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Tunapokea Malalamiko Ya Wananchi, Tunayafanyia Kazi – Dario
Habari July 2, 2025
VETA Mtwara Yawafundisha Wanafunzi Uongezaji Thamani Kwenye Korosho, Mwani
Habari July 2, 2025
VETA Shinyanga Yatumia Kompyuta Kubuni Bidhaa 
Habari July 2, 2025
Wafanyakazi Wa Majumbani  700 Wapatiwa Mafunzo VETA
Habari July 2, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?