MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Mdemu Azindua Utafiti Uliofanywa na FES Kwa Kushirikiana Na COTWU – T
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Mdemu Azindua Utafiti Uliofanywa na FES Kwa Kushirikiana Na COTWU – T
Habari

Mdemu Azindua Utafiti Uliofanywa na FES Kwa Kushirikiana Na COTWU – T

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
– Umegusa Changamoto, Vikwazo Vinavyowakabili Bodaboda

Na Lucy Ngowi

DAR ES SALAAM: MATOKEO ya Utafiti uliofanywa kuhusu Bodaboda wa Dar es Salaam, kuelekea Usafiri Endelevu na Uhakika wa Ustawi wa Maisha, utatambua mchango wa kiuchumi wa waendesha pikipiki wanawake hususan kwenye miji mikubwa.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Felister Mdemu amesema hayo wakati wa uzinduzi wa taarifa ya utafiti kuhusu waendesha Pikipiki Wanawake Mkoani Dar es Salaam.
Mdemu amesema utafiti huo pia utasaidia kutambua changamoto na vikwazo vinavyowakabili  katika kujikwamua kiuchumi.
Pia kutambua mahitaji ya wanawake waendesha pikipiki na mikakati ya kuongeza ushirika mpana wa kundi hilo.
Amesema lengo la serikali ni kuhakikisha inawawekea mazingira wezeshi na rafiki ili wafanyabiashara ndogo ndogo waweze kunufaika na fursa za kiuchumi na kijamii ikiwemo mikopo ya biashara kupitia Taasisi za fedha.
Amesema katika kukabiliana na changamoto zinazokwamisha maendeleo ya wafanyabiashara ndogo ndogo nchini, Wizara ya Maendeleo ya Jamii imeendelea na kazi ya kuratibu na kusimamia shughuli zao.
“Wafanyabiashara hao ni pamoja na wachuuzi wa bidhaa yaani machinga, mama/ baba lishe, waendesha bodaboda na bajaji, wasusi na wengine wote wenye mauzo ghafi yasiyozidi Sh. Milioni nne kwa mwaka.
“Utaratibu huu ubafanyika kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Wizara za kisekta pamoja na wadau.
“Hivyo matokeo ya utafiti huu ni ushahidi kuwa, serikali imedhamiria kushughulikia changamoto zinazolabili kundi hilo,” amesema.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Mawasiliano na Uchukuzi Tanzania  (COTWU – T), Juliana Mpanduji amesema kuwa ukuaji wa Sekta isiyo Rasmi ni muhimu kwani unalenga maisha ya mtanzania katika uzalishaji na kuongeza kipato.
Amesema utafiti huo umelenga hasa kuboresha mazingira ya uzalishaji ambao umekuwa ukikua kwa kasi.
” Kushirikiana na Friedrich Ebert Stiftung (FES) kwa mchango wao muhimu na kukubali kufanya kazi na sisi bega kwa began ni jambo kubwa nakupongeza sana.
” Hii inaonyesha upendo wa dhati kwa Tanzania, wanawake na wasafirishaji kwa ujumla.
” Hasa zaidi imegusa moyo wangu kama mwanamke ninayeongoza chama chenye wafanyakazi wanaume wengi,” amesema.
Amesema kwa sasa hiyo ni ajira kwa vijana na wanawake wengi wanaojikwamua kiuchumi.
Amesema tafiti hiyo iliyozinduliwa imeangazia mambo mengi ya maisha ya kila siku ya madereva kuhusu kipato chao, na changamoto za kazi hiyo kwa kuwa mara nyingi haichukuliwi kama ni kazi yenye staha.

You Might Also Like

Katibu Mkuu CCM Dkt. Nchimbi Akutana na Katibu Mkuu CRC

Utekelezaji Mradi Mkubwa Wa Maji Mwanza Wafikia Asilimia 35

CCCC Yaandaa Tamasha La Dragon Boat

Mitambo 10 Ya Uchimbaji Madini Yenye Thamani Ya Bilioni 10 Yazinduliwa

Polisi Kuimarisha Ulinzi Nyumba Za Ibada Krismasi, Mwaka Mpya

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Kwelea Kwelea, Nzige, Viwavi Jeshi Kudhibitiwa Kwa Haraka
Next Article Mpanduji Wa COTWU – T Aelezea Changamoto Zinazowakabili Waendesha Bodaboda, Bajaji
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?