MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Chalamila Atoa Wiki Mbili Wafanyabiashara Ndogo Ndogo Kufungua Njia Kariakoo
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Chalamila Atoa Wiki Mbili Wafanyabiashara Ndogo Ndogo Kufungua Njia Kariakoo
Habari

Chalamila Atoa Wiki Mbili Wafanyabiashara Ndogo Ndogo Kufungua Njia Kariakoo

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Lucy Ngowi

DAR ES SALAAM: MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameuagiza uongozi wa Wafanyabiashara Ndogo Ndogo kuanza kufungua barabara zinazoingia sokoni Kariakoo ili magari yaweze kupita.

Chalamila ametoa agizo hilo leo jijini Dar es Salaam  alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu ufunguaji wa soko hilo.

“Leo utakapokwenda soko hilo njia zake karibu zote zimefungwa na zimefungwa na wafanyabiashara ndogo ndogo ambao wameweka meza katika maeneo ya barabara na kwa mantiki hiyo kuzuia uingiaji wa magari makubwa sababu unakuta bado kuna shughuli za uingizaji wa mizigo mikubwa ndani ya soko.

“Nitoe rai kwamba uongozi wa wafanyabiashara ndogo ndogo eneo la Kariakoo waanze kufungua barabara hizi ili magari yatakapoanza kupita, mwisho wa siku soko litakapozinduliwa kusiwe na msongamano wa aina yoyote kuhusu kuingia ama kutoka kwa barabara za hiyo njia.

“Wafanya biashara hao wako watu watakaoniuliza watakwenda wapi, wafanyabiashara wote na hasa wafanyabiashara ndogo ndogo katika lile soko jipya ambalo limejengwa tumeratibu menejimenti ya shirika la soko Kariakoo wataeleza,

“Limeratibu kadri watakavyozidi kupanda sakafu ya kwanza kwenda mpaka ya tatu hadi ya nne kutakuwa na vijiduka vidogo vidogo ambavyo wafanyabiashara wa biashara ndogo ndogo watapangwa.

“Sasa Natoa muda wa wiki mbili ili uongozi wa Machinga katika eneo la Kariakoo waweze kukaa na wafanya biashara ndogo ndogo wawaeleze kuhusu azma ya serikali na namna ya kufungua njia  ili mwisho lisije likawa soko ambalo halina tija kwa uwekezaji mkubwa ambao umeshafanywa sasa,” amesema.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Kariakoo, Ashraph Abdulkarim amesema shirika limejipanga kutangaza maeneo yaliyo wazi ili wafanyabiashara waweze kuyaomba, jambo litakalofanyika ndani ya siku saba.

Amesema wamejipanga kutangaza maeneo ya biashara yaliyowazi katika soko hilo,  Juni mbili mwaka huu 2025.

“Tutatangaza maeneo hayo kwa wafanyabiashara wote na wananchi wenye nia ya kufanya biashara katika soko la Kariakoo tunawakaribisha.

“Muwe tayari ndani ya siku saba tutafanya uchambuzi wa wale watakaokuwa wamepata ili tuweze kuendelea na biashara,” amesema.

Amesema kwa wafanyabiashara waliokuwepo awali katika soko hilo kabla halijaungua wanamalizia kufanya uhakiki kwa wale ambao walikuwepo lakini wamefariki, kwa hiyo kuna taratibu za mirathi za kufuata kupitia Kamati ya mirathi.

Pia kuna maelekezo ya wale waliokuwa wanadaiwa kabla ya soko halijaungua kwa  hao tunawapigia simu na kuwaelekeza tena nini cha kufanya.

Amesema sakafu ya kwanza kutakuwa na mboga mboga  na kila sakafu itakuwa na biashara tofauti na nyingine, sakafu ya tatu, nne na tano kutakuwa na viuatilifu, nafaka na vifungashio.

Pia kuna maeneo ya migahawa hivyo wanaohitaji kufanya biashara hiyo wafike pindi litakapotolewa tangazo.

You Might Also Like

Kanisa lakabidhi jengo la watoto la milioni 595 kwa serikali

Maeneo ya hifadhi yalindwe na kutunzwa – Rais Samia

Majaliwa  awataka waandamizi, vyombo vya usalama kutekeleza 4R

Msigwa Awataka Wakuu Wa Mikoa Kuandaa Maeneo Ya Upandaji Miti

Rais Samia Kushiriki Mkutano Wa Wakuu Wa Nchi Ethiopia

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Mtanda Akagua Maendeleo Ya Mradi YA Hoteli Ya Nyota Tano Ya NSSF
Next Article Miaka Minne Ya Samia Na Sekta Ya Elimu
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Rais CWT Asikitishwa Na Uzembe, Maofisa Wa Halmashauri
Habari July 20, 2025
Rais Mpya CWT Ikomba: ‘Nataka Kuwaunganisha Walimu, Kuitendea Haki Kazi Yetu’
Habari July 20, 2025
Tumeleta Utulivu na Huduma kwa Walimu’ – Ikomba
Habari July 20, 2025
Afya Bora Yachochea Ustawi wa Wananchi Kigoma
Habari July 20, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?