Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: BODI ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), imetoa mwezi mmoja mwezi mmoja kuanzia Mei 22 hadi Juni 21, mwaka huu kuomba kuthibitishwa na kupewa vitambulisho kwa Waandishi wote wanaofanya kazi ya kihabari nchini.
Usajili huo unafanyika kupitia Mfumo wa TAI – Habari.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JAB, Patrick Kipangula amesema hayo katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari.
“Waandishi wanapaswa kujisajili kupitia kiunganishi kilichotolewa na JAB,
Vile vile amesema kutokana na uwepo wa uchaguzi Mkuu mwaka huu, waandishi wote wa habari watakaotekeleza majukumu ya kihabari yanayohusiana moja kwa moja na mchakato huo wa uchaguzi wanapaswa kuwa wamethibitishwa na bodi hiyo,
“Bodi inahimiza Waandishi wa Habari kutumia ipaswavyo muda uliotokLewa kujisajili na kupata vitambulisho,” amesema