Na Danson Kaijage
JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) imezindua kampeini maalumu ya Kijani Fact Scan yenye lengo la kutetea ukweli katika Taifa na kutokomeza upotoshaji na uongo.
Hayo yameelezwa na Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa Jessica Mshana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mohamed Kawaida katika ukumbi wa mikutano wa umoja huo Jijini Dodoma.
Jesca amesema kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi kumekuwepo na tabia kubwa ya upotoshaji na kauli za kuichafua Serikali na chama tawala jambo ambalo kwa sasa linaenda kujibiwa na kampeini hiyo maalum.
“Katika kipindi cha hivi karibuni kumekuwepo na ongezeko la taarifa za upotoshaji dhidi ya Serikali,viongozi ,chama cha mapinduzi na Jumuiya zake hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu.
“Kwa masikitiko makubwa ,upotoshaji unaofanywa na baadhi ya wanaharakati ,baadhi ya wanasiasa na hata baadhi ya watu kutoka ndani na nje ya nchi kwa makusudi ya kupotosha Umma ,kuchafua taswira ya taifa na kuvuruga amani ya nchi na mshikamano wa kijamii kampeini hiyo itafanya kazi kubwa ya kujibu upotoshaji huo kwa hoja,” amesema Jesca.
Amesema kampeini hiyo itafanya opareisheni ya kizalendo ya kukabiliana na upotoshaji na kupitia KijaniFactScan itahusika kutoa taarifa sahihi na elimu kwa Umma juu ya taarifa potofu zinazozunguka na njia ya kukabiliana nazo.
Aidha amesema kuwa kampeini hiyo itahusika kujibu hoja kwa hoja kwa kutumia ushahidi,Takwimu na tafsiri sahihi.
Jesca ameeleza kuwa kampeini hiyo itahakikisha propaganda chafu na kuziba mianya yote ya upotoshaji pia ataahirikishwa kila kijana na kila mwana jamii mzalendo kuwa sehemu ya ulinzi wa Taifa dhidi ya upotoshaji.
Katika hatua nyingine amesema Mei 23 mwaka huu UVCCM Taifa watakuwa na baraza kuu maalum jijini Dodoma