MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Senyamule Ahamasisha Ushiriki Wa Vijana Katika Uchaguzi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Senyamule Ahamasisha Ushiriki Wa Vijana Katika Uchaguzi
Habari

Senyamule Ahamasisha Ushiriki Wa Vijana Katika Uchaguzi

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Danson Kaijage
DODOMA: MKUU wa Mkoa wa Dodoma,  Rosemary Senyamule, amesema michezo inaweza kuwa daraja muhimu la kuwahamasisha vijana kushiriki katika mchakato wa kidemokrasia, hususan kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Akizungumza wakati wa fainali ya Polisi Jamii Cup kati ya timu za Mpunguzi na Chang’ombe, Senyamule amesema mashindano hayo si tu burudani bali pia ni chombo cha malezi ya uzalendo, nidhamu na ushiriki wa kijamii.
“Michezo siyo tu ushindani wa uwanjani. Ni darasa la maisha. Hapa vijana wanajifunza mshikamano, uvumilivu, na uzalendo—nguzo kuu za uchaguzi wa amani,” amesema.
Amesema Mkoa wa Dodoma utaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kutumia michezo kama jukwaa la kutoa elimu ya uraia, kuhimiza usalama wa jamii na kuhamasisha vijana kujitokeza kujiandikisha na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi.
“Rais Samia ameendelea kuwekeza kwa vijana kupitia michezo na programu mbalimbali. Tunapowaona vijana wakijitokeza kama hawa wa Polisi Jamii Cup, tunaona picha ya Taifa lenye matumaini,” amesema.
Amewataka vijana kutumia nafasi ya sasa sio tu kujiandikisha kama wapiga kura bali pia kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, huku akisisitiza umuhimu wa kuepuka kauli na vitendo vinavyoweza kuvuruga amani.
Kwa  upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi, George Katabazi amesema  mashindano ya Polisi Jamii Umoja Cup yamehusisha jumla ya timu 14 kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa huo, kwa lengo la kuimarisha mahusiano kati ya Jeshi la Polisi na wananchi.
Amesema kupitia mashindano hayo, Jeshi la Polisi linakusudia kujenga uelewa na ushirikiano wa karibu na jamii ili kuhakikisha wanajiepusha na vitendo vya kihalifu pamoja na kushiriki kikamilifu katika utoaji wa taarifa kuhusu uhalifu na wahalifu.
“Tunatumia michezo kama jukwaa la kuleta mshikamano, kuwahamasisha vijana kuepuka uhalifu na kuwa sehemu ya suluhisho kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kulinda amani ya maeneo yao,” amesema Katabazi.

You Might Also Like

Endeleeni Kuunganisha Mifumo Ya TEHAMA Ya Kisekta – Kakoso

Majaliwa ataka kuondolewe vikwazo vya rufaa za matibabu Afrika Mashariki

Mkurugezi Mkuu LATRA, Kamanda Ng’anzi Wafanya Ukaguzi Wa Kushtukiza Stendi Ya Magufuli

Shemdoe aridhika huduma zinazotolewa na TVLA nanenane

Nchimbi Agongelea Nyundo Kwa Wagombea Watoa Rushwa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Polisi Dodoma Yawataka Wananchi Kutoa Taarifa 
Next Article Dkt. Ndumbaro : Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Imefanikiwa 
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

‘Jichunge’ Programu Ya Simu Yenye Mafanikio Katika Kuboresha Matumizi Ya Dawa Kinga Dhidi Ya VVU
Habari July 7, 2025
Toleo La Sheria Zilizotafsiriwa Kwa Kiswahili Kutoka Agosti
Habari July 7, 2025
Waendelezaji Majengo 103 Kesi Ziko Mahakamani, -AQRB
Habari July 6, 2025
TSB Yatangaza Fursa Za Kilimo, Uwekezaji Wa Mkonge
Habari July 6, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?