Na Waandishi Wetu
Inaonekana kwamba vita vya ushuru wa forodha duniani vilivyoanzishwa na Donald Trump vinasababisha Marekani kujitenga kwenye jukwaa la uchumi wa kimataifa.
Msemaji wa serikali ya Ufaransa alikuwa wa kwanza kutoa tuhuma kali za kidiplomasia dhidi ya Marekani kwa kumkosoa Trump kwa kuchukua ,’msimamo wa kibeberu’.
Hili linadhihirisha kuwa mpasuko mkubwa umejitokeza katika uhusiano kati ya Marekani na washirika wake kutokana na sera ya ushuru.
Marekani imeongeza ushuru wa forodha kwa Ulaya na kudai malipo ya ulinzi zaidi, huku ikichukua hatua peke yake katika suala la Urusi na Ukraine.
Vitendo hivi vimeharibu vibaya maslahi ya washirika wake.
Kutokana na hatua iliyochukuliwa na Marekani kuhusiana na ushuru wa forodha, imesababisha nchi mbalimbali kupinga.
Nchi ya China ilikuwa ya kwanza kuchukua hatua za kupambana, ikaongeza ushuru wa asilimia 34 kwa bidhaa za Marekani na kutekeleza udhibiti mkali wa mauzo ya nje kwenye eneo la madini.
Umoja wa Ulaya nayo ilipinga hatua hiyo ya Marekani.
Vile vile Uingereza, Australia na nchi nyingine zimeonyesha kutoridhika na sera za ushuru wa forodha ya Marekani.
Nayo Singapore ambayo inategemea sana biashara ya kimataifa, pamoja na nchi za Asia kama Japan, Korea Kusini, Thailand, Vietnam na nyinginezo, zote zinakumbana na hasara kutokana na sera mpya za ushuru wa forodha za Marekani, hivyo zinaomba kujadili jinsi ya hatua za kukabiliana na hali hiyo.
Afrika Kusini, kama nchi iliyoendelea zaidi kiviwanda Barani Afrika, imeathiriwa sana na sera za ushuru wa forodha za Marekani.
Marekani inatoza ushuru wa asilimia 30 wa forodha kwa bidhaa za Afrika Kusini, na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alijibu kwa kusema ushuru wa kulipiza kisasi uliowekwa kwa upande mmoja ni kizuizi cha biashara na ustawi wa pamoja.
Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Ronald Lamola amesema sera za ushuru wa forodha za Donald Trump zimepunguza faida zilizoletwa na Sheria ya Ukuaji na Fursa ya Afrika (African Growth and Opportunity Act – (AGOA), na zinaweza kusababisha kukomeshwa kwa sheria hiyo.
Sheria ya AGOA ilianza kutekelezwa mwaka 2000. Inaruhusu nchi za Afrika zinazostahiki kuuza bidhaa zaidi ya aina 1000 kwa Marekani bila kutozwa ushuru.
Hivi sasa, nchi 39 za Afrika zinanufaika nayo.
Mwaka 2002, thamani ya mauzo ya Afrika kwa Marekani yalifikia takriban dola za kimarekani bilioni 28, ambapo mauzo ya bidhaa chini ya Sheria ya AGOA yalichangia takriban asilimia 30.
Lakini Rais Trump amedokeza mara nyingi kuwa hatakubali tena kusaini upya AGOA, akikosoa sheria hiyo kwa kushindwa kuletea Marekani faida ya kuridhisha.
Ikiwa sheria hii itasitishwa, uchumi wa nchi za Afrika ambao unategemea mauzo ya nje kwa Marekani utapata hasara kubwa.
Rais Donald Trump amedokeza mara nyingi kuwa hatakubali tena kusaini upya AGOA, akiikosoa sheria hiyo kwa “ kushindwa kuletea Marekani faida ya kuridhisha.”
Ikisitishwa Sheria ya AGOA, Tanzania itakabiliwa na hasara kubwa za uuzaji nje ya nchi , upotezaji wa ajira katika sekta husika na upunguaji wa uchumi.
Kama nchi muhimu kiuchumi katika Afrika Mashariki, Tanzania inaweza kukumbana na shinikizo la ushindani wa kikanda kutokana na uhamishaji wa biashara.
Katika muktadha huu, ujenzi wa pamoja wa “Jumuiya ya Ngazi ya Juu yenye Mustakabali wa Pamoja” kati ya China na Tanzania unaonekana kuwa na umuhimu zaidi.
hiyo ni kupitia Mpango wa “Mkanda Mmoja, Njia Moja”, China inaendelea kusaidia maendeleo ya miundombinu, nishati na sekta nyingine za Tanzania, huku ikikuza uanuwai wa biashara duniani.
Inadhihirisha kuwa Tanzania inatakiwa kuimarisha ushirikiano wa kivitendo na China katika nyanja mbalimbali na kupunguza utegemezi wake kwa soko moja tu, ili kupata maendeleo endelevu katika hali ya usawa na ya kunufaishana.
Mwandishi Ning Yi, mwalimu wa Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU).
Barua pepe:02706@shisu.edu.cn
Mwandishi Ye Tianfa, mwalimu wa Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Tianjin (TFSU)
Barua pepe: tianfa202123@163.com