MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Waajiri Wasilisheni Michango Kwa Wakati
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Waajiri Wasilisheni Michango Kwa Wakati
Habari

Waajiri Wasilisheni Michango Kwa Wakati

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read

Na Mwandishi Wetu

TANGA: WAAJIRI wa sekta binafsi wametakiwa kuzingatia wajibu wao wa kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwa wakati ili kuwawezesha wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kupata mafao yao kwa mujibu wa sheria.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF, Mwamini Malemi ametoa wito huo, wakati akizindua rasmi Mkutano wa 54 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Mfuko huo.

Malemi amesema michango ya waajiri ni uti wa mgongo wa uendeshaji wa Mfuko, hivyo kucheleweshwa kwake kunaathiri moja kwa moja ustawi wa wanachama na ufanisi wa utoaji huduma za mafao.

“Naomba nitumie nafasi hii kuwaasa waajiri wote kuhakikisha wanawasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati.

“Hili si jambo la hiari bali ni wajibu wa kisheria unaolenga kulinda haki za wafanyakazi,” amesema.

Ameongeza kuwa, NSSF inaendelea kutoa huduma bora na endelevu kwa wanachama wake kwa kuzingatia misingi ya uadilifu, uwajibikaji na matumizi ya teknolojia ili kuongeza uwazi na ufanisi katika shughuli za kila siku.

Akizungumza kuhusu mafanikio ya Mfuko, Malemi amesema NSSF imeendelea kuwa taasisi ya mfano katika sekta ya hifadhi ya jamii kwa kuimarisha mifumo ya TEHAMA, kuongeza kasi ya uandikishaji wanachama, kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato na kufanya uwekezaji wenye tija.

“Lengo letu ni kuhakikisha kila mwanachama anaendelea kupata huduma bora, ya kisasa na inayokidhi matarajio.

“Tunataka NSSF iwe taasisi ya mfano katika uwajibikaji,” amesema.

Pia amewapongeza wajumbe wapya wa Bodi ya Wadhamini na kuwataka kuhakikisha Mfuko unasimamiwa kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo iliyowekwa, huku akiwataka wajumbe wa Baraza hilo kuwa chachu ya mabadiliko chanya katika maeneo yao ya kazi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, amesema Mfuko unatarajia kupata mafanikio makubwa zaidi kwa kuwa umewekewa vipaumbele vinavyolenga kupanua wigo wa wanachama,

Pia kuongeza mapato, kuboresha ulipaji wa mafao na kuimarisha huduma kwa wanachama kupitia mifumo ya TEHAMA.

Awali, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala, Ekwabi Mujungu aliwataka wajumbe wa Baraza hilo kuzingatia kwa makini maazimio watakayoyapitisha ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Mfuko.

Flora Ndutta akitoa neno la shukrani amesema NSSF itaendelea kutoa huduma bora kwa kutumia TEHAMA, kuwafikia wananchi waliojiajiri na kwamba wataendelea kufanya kazi kwa bidii, kwa weledi na kwa kuzingatia maadili.

You Might Also Like

Dkt. Ndumbaro : Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Imefanikiwa 

Sierra Leone Yaipongeza TARURAUjenzi Wa Madaraja, Barabara Za Mawe

Sera mpya ya viwanda kuzinduliwa

Wagonjwa 472 Waonwa Na Daktari Wa Mifupa MOI, 40 Wapendekezwa Kufika Dar kwa Matibabu

Mgodi Wa Dhahabu Wa Nyanzaga Kunufaisha Wananchi, Ujenzi Wazidi Kupaa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article China Yaendelea Kunufaisha Afrika, Wakati Marekani Ikikatiza Uwekezaji Katika Bara Hilo
Next Article Trump Kusitisha Sheria Za AGOA, Afrika Yapata Hasara
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Madaktari Kutoka Ireland Watoa Matibabu Ya Mifupa Kwa Watoto MOI
Habari October 20, 2025
Mwalim: Nikichaguliwa urais, Kigaila atakuwa Waziri Mkuu wangu
Habari October 20, 2025
ARTICLE 19,  JOWUTA KUSHIRIKIANA KUIMARISHA HAKI ZA WANAHABARI
Habari October 18, 2025
Profesa Ndunguru Aongoza Kikao Cha Mawaziri Wa DLCO- EA Akimwakilisha Bashe
Habari October 17, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?