Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 7, 2026
Habari Lucy Ngowi 6

Matokeo Ya Usaili TRA Kutangazwa April 25,2025

Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema matokeo ya usaili wa maandishi kwa watahiniwa walioomba nafasi za kazi katika Mamlaka hiyo, yatatangazwa Aprili 25  mwaka huu.
Imesema matokeo hayo ya usaili uliofanyika  Machi 29 na 30 mwaka 2025  yatatangazwa kupitia Tovuti ya TRA (www.tra.go.tz) baada ya kuwasilishwa na Mshauri elekezi Aprili 23, mwaka huu.
Akizungumzia mchakato huo wa ajira za TRA  Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimali watu na Utawala  Moshi Jonathan Kabengwe amesema baada ya majina kutangazwa Mei 2 hadi 4  utafanyika usaili wa Vitendo kwa Madereva na Waandishi Waendesha Ofisi.
Amesema baada ya Usaili wa Vitendo utafuata Usaili wa mahojiano kwa kada nyingine ambao utafanyika kwa siku tatu kuanzia Mei 7 hadi 9  2025 ambapo watakaofanikiwa kushinda Usaili huo wataarifiwa  Mei 18,.2025 na kuanza mafunzo Elekezi Mei 22,2025 mpaka  Juni  02,2025 watakapoajiriwa na kuanza kazi rasmi.
 Kabengwe ameeleza kuwa katika mchakato wa usaili maombi yaliyokidhi vigezo yalikuwa 112,952 yakaongezeka maombi 71 baada ya kukata Rufaa na kufikisha idadi ya maombi 113,023 yaliyohusisha waombaji 86,314 na waliofanya Usaili wa maandishi ni waombaji 78,544 sawa na asilimia 91 ya waombaji wote na waombaji 7,770 sawa na asilimia tisa hawakufika kwenye Usaili kwa sababu mbalimbali.
Ameeleza kuwa Sera ya TRA ni ajira sawa kwa wote na ajira zilizotangazwa zitazingatia sifa na vigezo vya muomba kazi bila kujali hali ya muhusika kwamba ni Mtoto wa Maskini, Mtoto wa Kiongozi au Mtoto wa Mtumishi wa Umma ndiyo maana vituo vya Usaili viliwekwa kwenye mikoa nane na Zanzibar ili kusogeza huduma karibu.
Aidha  Kabengwe ameshukuru kuwepo kwa mrejesho kutoka kwa Jamii kupitia njia mbalimbali na kueleza kuwa kama yupo mwenye Taarifa zinazoashiria kuharibu zoezi la ajira awasiliane na TRA kupitia Sikika App, namba za Simu Bure 0800 750 075 / 0800 780 078 / 0800 110 016 au Whatsapp  0744 233 333 au E-mail huduma@tra.go.tz / services@tra.go.tz au atoe Taarifa TAKUKURU
Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.