MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Ujenzi Jengo la Sayansi, Teknolojia, Ubunifu Kuanza Kesho Dodoma
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Ujenzi Jengo la Sayansi, Teknolojia, Ubunifu Kuanza Kesho Dodoma
Habari

Ujenzi Jengo la Sayansi, Teknolojia, Ubunifu Kuanza Kesho Dodoma

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: UJENZI wa jengo la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu la Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ( COSTECH), unaanza kesho Machi 26, 2025 baada ya mkandarasi kukabidhiwa rasmi eneo la mradi.
Mkandarasi wa jengo hilo ni TIL Construction Limited.
Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), kutoka COSTECH, Dkt. Aloyce Andrew amesema hayo jijini Dodoma baada ya kukabidhi eneo hilo kwa mkandarasi TIL Construction Limited.
Dkt. Andrew amesema wamekabidhi eneo hilo kwa mkandarasi kwa lengo la kuanza ujenzi wa jengo hilo.
“COSTECH ina jengo Dar es Salaam lakini inatarajia kujenga Dodoma kwa ajili ya kurahisisha utoaji huduma kwa wadau wetu.
“Jengo hilo litakuwa na sehemu ya kuhudumia wabunifu, sehemu ya kuatamia kampuni changa, pia sehemu ya kuratibu masuala ya utafiti,” amesema.
Amesema ujenzi huo unatarajia kukamilika ndani ya miezi 12 tokea waliposaini mkataba jana Machi 24, 2025 mkoani Dar es Salaam.
Kwa upande wake Mshauri Elekezi kutoka Kampuni ya MEKON, Benedict Martin amesema wamekuwepo kwa ajili ya kumkabidhi mkandarasi eneo hilo la ujenzi.
“Tulianza ku design eneo toka mwaka jana baada ya mteja wetu COSTECH kutuonyesha eneo hili ambalo lina mita za mraba 4800, ukubwa wa mita 80 kwa 60 na michakato ya ku design ilianza toka mwaka jana tulipopata zabuni.
” Tumeshirikiana na COSTECH kupata jengo litakalokidhi matakwa yao yote pia tuna uhakika wa mkandarasi tuliyempata amekidhi vigezo.
“Tunaamini mradi utakamilika bila itilafu yoyote,” amesema.
Amesema katika zabuni ya ujenzi kulikuwa na washindani 12, lakini TIL imeshinda kutokana na miradi iliyofanya kabla na kukidhi vigezo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya ujenzi TIL, Ding Fubing amesema baada ya kukabidhiwa eneo la mradi wanaanza rasmi ujenzi kesho.
“Tupo kwa ajili ya kukabidhiwa eneo ili tuanze kazi. Baada ya kukabidhiwa tunaanza ujenzi rasmi kesho kwa kuanza kulisafisha eneo lote, na baada ya wiki mbili au tatu tutaanza sasa ujenzi rasmi baada ya kukubaliana na mshauri,” amesema.
Amesema,”Wategemee tutafanya kazi nzuri tutaimaliza kazi hii ndani ya muda au kabla ya muda. Vyote vitategemeana na ule ushirikiano tutakaokuwa nao pamoja,”.
Akizungumza kwa niaba ya COSTECH, Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi, Imanuel Mgonja amesema wapo na mshauri elekezi Kampuni ya MEKON ambaye atakuwa msimamizi wa jengo hilo.
Amesema naye Mkandarasi Kampuni ya TIL ameahidi ataifanya kazi hiyo kwa wakati na ubora unaotakiwa.
“Kwa niaba ya COSTECH tunawashukuru mshauri elekezi na mkandarasi kwa sababu wanaonyesha wana nia ya kufanya kazi kwa ubora unaotakiwa,” amesema.

You Might Also Like

Wakulima wametakiwa kuzingatia matumizi sahihi ya mbolea

Kamati Ya Bunge Yaipongeza TVLA Uzalishaji wa chanjo

Serikali Yaja Na Kanuni Mpya Ya Sheria Ya Fidia   Kuboresha Mazingira Ya Mfanyakazi 

Hospitali ya Temeke kufanyiwa maboresho eneo la huduma Kwa wateja

Rais Samia Awasili Mwanza Kilele Cha Mbio za Mwenge

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article WMA Yajivunia Kuongezeka Kwa Wafanyakzai
Next Article Waziri Kombo: Ushirikiano Wa China, Tanzania Umeleta Maendeleo Ya Kijani
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Tume ya Kurekebisha Sheria Yaelimisha Umma Kuhusu Haki za Wanyama
Habari August 6, 2025
Bundi Wasaidia Kupambana na Panya: Teknolojia Asilia Inayobadili Maisha ya Wakulima
Habari August 6, 2025
Ofisa wa TARI Kuwapo Kila Kituo cha Umwagiliaji – Naibu Katibu Mkuu
Habari August 6, 2025
Mbinu Mpya za Kilimo kwa Vijana Zapata Umaarufu Nanenane Banda La VETA
Habari August 6, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?