MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: COSTECH Yasaini Mkataba Ujenzi Jengo La Sayansi, Teknolojia, Ubunifu
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > COSTECH Yasaini Mkataba Ujenzi Jengo La Sayansi, Teknolojia, Ubunifu
Habari

COSTECH Yasaini Mkataba Ujenzi Jengo La Sayansi, Teknolojia, Ubunifu

Author
By Author
Share
2 Min Read

Na Lucy Ngowi

DAR ES SALAAM: TUME ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), imesaini mkataba na Kampuni ya TIL Construction Limited kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Jengo la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STI) Complex jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Amos Nungu amesema kuwa ujenzi huo ni sehemu ya Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.

Dkt. Nungu amesema katika mradi huo COSTECH wametengewa Sh. Bilioni 18 ambazo zitatumika kwa ajili ya kuimarisha na kuboresha menejimenti ya mifumo elimu ya juu katika kuwezesha mageuzi ya elimu kiuchumi pamoja na kuboresha miundo mbinu ya COSTECH.

“Kwa hiyo tunafanya ukarabati hapa jengo la makao makuu Dar es Salaam, tumeshapata mkandarasi, tumeshapata vibali pia tunajenga jengo Dodoma,” amesema.

Amesema kiasi hicho cha fedha Sh. Bilioni 18, jumla ya Sh. Bilioni 8 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la STI Complex na ukarabati wa jengo lililopo.

Amesema ujenzi huo utajengwa kwa miezi 12 ukikamilika makao makuu ya tume hiyo yatakuwa Dodoma.

“Dar es Salaam na Zanzibar zitabaki kuwa ofisi za Kanda. Ujenzi ukikamilika tutanunua vifaa vya kisasa kwa ajili ya kuhakikisha ni usaidizi unaotakiwa kuelekea mageuzi makubwa ya kiuchumi,” amesema.

Amesema wana imani jengo hilo litakamilika ndani ya wakati, “Tutapatikana muda wowote tutakaohitajika kuhakikisha kazi haisimami,”.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TIL, Ding Fubing amesema watafanya jitihada zao zote kuhakikisha mradi huo unakamilika ndani ya muda waliopewa.

You Might Also Like

Tanzania Yazindua Mkakati wa Taifa wa Usimamizi Na Uendelevu wa Mikoko

Mgombea Urais CHAUMMA Asema Nchi Inahitaji Mawazo Mapya

Ikomba: Aliishi Na Watoto Wiki Sita Akiwafundisha Kabla Ya Mtihani WaTaifa

Mapinduzi ya Elimu Geita: Wasichana Wamerudi Shule kwa Kasi

Mpango Mkakati wa Takwimu wazinduliwa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article NEMC Kupambana Na Magugu Maji Ziwa Victoria
Next Article Wakulima Wa Mahindi Mvomero Walia Na Viwavijeshi Vamizi, Watafiti SUA kupitia Mradi Wa AGRISPARK Kuokoa Jahazi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Waziri Mkuu Majaliwa Akabidhi Tuzo kwa BoT Geita
Habari September 22, 2025
BoT Yarahisisha Uuzaji wa Dhahabu kwa Wachimbaji, Yatoa Punguzo La Mrabaha
Habari September 22, 2025
Waziri Mkuu Apongeza Huduma Kidijitali za NSSF, Maonesho Ya Madini Geita
Habari September 22, 2025
Mkuu Wa Mkoa Shinyanga Asifu Kazi Ya Bodi Bima Ya Amana
Habari September 22, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?