Na Danson Kaijage
DODOMA: OFISI ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA)imesema kwa kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita imefanikiwa kupokea migogoro 13, kusuluhisha 118 ambapo 10 kati ya hiyo haikumalizika.
Migogoro hiyo ambayo haikumalizika ilifunguliwa kesi mahakamani, mingine nane inaendelea kushughulikiwa.
Hayo yameelezwa Jijini Dodoma na Ofisa Mtendaji Mkuu na msimamizi wa hakimiliki, Doreen Sinare alipozungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO kuhusu mafanikio ya miaka minne ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema kupolelewa kwa mogogoro hiyo kumatokana na uelewa wa wasanii na wadau mbalimbali kutambua umuhimu haki miliki zao jambo ambalo halikuweza kujitokeza kwa miaka ya nyuma.
Amesema kwa miaka minne sasa wasanii wote pamoja wadau mbalimbali waliopo chini ya Cosota wameweza kutambua haki zao, umuhimu na faida ya chombo hicho.
Akiendelea kutaja mafanikio mbalimbali ya kuwepo kwa COSOTA kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa sasa, amesema ni pamoja na muziki wa singeri kutambuliwa ndani na nje ya Tanzania.

Amesema kutambuliwa kwa muziki huo, kwa sasa umekiwa ukitumiwa na watu mbalimbali ikiwapo kuhamasisha shughuli za kimaendeleo tofauti na ilivyokuwa
miaka ya nyuma.
Vile vile amesema kupitia Kanuni ya Tozo ya Hakimiliki mapato hayo yalianza kukusanywa.
Ameeleza kuwa kupitia chanzo hicho COSOTA imekusanya Sh. Bilioni 1.4
kuanzia Septemba, 2023 hadi Februari, 2025 ambapo Ofisi imefanikiwa kupokea fedha za tozo ya hakimiliki za mwaka wa fedha 2023/2024 kutoka Wizara ya Fedha kiasi cha Sh. Milioni 847.