Na Lucy Lyatuu
SERIKALI imesema gridi ya taifa ni dhaifu sana kwa mikoa ya Kaskazini ikisababisha kushuka kwa voltage na kwamba mara nyingi inapozimika huanzia mikoa hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Felchesm Mramba amesema hayo Dar es Salaam akitoa ufafanuzi kuhusu Tanzania kununua umeme kutoka Nchini Ethiopia kwa ajili ya mikoa ya Kaskazini.
Amesema sekta ya Nishati wanamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi na ridhaa ya kuruhusu umeme kuingia kanda ya kaskazini kutokea nchi jirani.
“Ni uamuzi sahihi mno kwa sababu wananchi wanaolia kwa kuwa na umeme mdogo watakuwa wamefanikiwa na pia upotevu wa umeme unaotokea kule Kaskazini utakuwa umeokolewa,” amesema.
Amesema hali ya umeme nchini sio kwamba hakuna changamoto lakini uzalishaji umeme wa kutosha nchini upon a kwamba hauchukuliwi kwa sababu kuna upungufu nchini.
Amesema sababu ya kuchukua umeme kwa ajili ya kaskazini ni kwamba hali ya umeme katika mikoa y akaskazini ambayo ni Kilimajnaro Arusha Manyara na Tanga ni kutokana na grid hiyo kuwa dhaifu.
“Umeme tunaozungumzia kwamba tunataka kuuchukua kwa Kaskazini ni kidogo sana sio mwingi ni Megawati 100 pekee na Mahitaji yote ya Kaskazini Megawati 700,” amesema
Amesema kwa sasa umeme unaozalishwa nchini ni Megawati 3796 na umeme unaohitajika nchini Megawati 2200 na kusababisha kuwa na salio kubwa, kuna umeme mwingi wa ziada.
Mramba amesema mfumo w aumeme una vitu zaidi ya kimoja kwamba kiasi cha umeme n ahata ubora wa umeme,
Amesema kwa mikoa ya Kaskazini changamoto kubwa iliyopo kule ni kushuka kwa voltage ambapo husababisha taa kuwaka kama kibatari.
Amesema tatizo ni kubwa sana huko na sababu hiyo huanzia pale umeme unapoanzia hadi kwa mtumiaji iwapo umbali ni mrefu voltage hupugua mpaka unapofika.
“Kwa Tanzania umeme wetu mwingi huzalishwa mikoa ya kusini, kama Dar es Salaam, Pwani Morogoro na kama mteja yuko Manyara inabidi kusafiri kwenda huko hivyo voltage hupungua njiani na zinaposhuka husababisha upotevu wa umeme,” amesema.
Amesema ili kutatua changamoto hiyo ni kuweka chanzo cha kuzalisha umeme kwenye mikoa hiyo kuingiza umeme kwenye mikoa hiyo kutokea kwenye mifumo mingine na Tanzania imepata umeme kutokea nchini Ethiopia na kuingilia Namanga mkoani Arusha.
Amesema umeme utakapoingizwa pale ambao ni Megawati 100 utasababisha voltage inayokuw aimeshuka kupanda na kurudi kwenye kiwango chake na ule upotevu wa umeme unaopotea kule utaokolewa.
Amesema kwa kufanya hivyo wananchi wanaolia voltage kushuka , mfumo mzima utarudi kawaida na kutumika ipasavyo.
Aidha amesema upotevu wa umeme unaopotea kule kaskazini, Megawati 17 zitakuwa salama. Ule umeme unaotakiwa kuingizwa sio jambo la ajabu na nchi na nchi kuuziana umeme sio jambo la ajabu.
Amefafanua kuwa Tanzania inanunia umeme nchi tatu ambazo ni Zambia ambao umeme wake unatumika mkoa wa Rukwa, Uganda na umeme wake hutumika mkoa wa Kagera na Kenya ambapo umeme wake hutumika eneo la Horohoro wilaya ya Mkinga.
Kuhusu umbali wa kuingiza umeme kutoka Ethiopia amesema sio kwamba unachukuliwa kule moja kwa moja bali mita itaunganioshwa na nchi ya Kenya ambapo utapita na kuunganishwa eneo la Namanga.
“Kati ya sisi na Ethiopia lazima kuishirikisha Kenya, kwamba wao Ethiopia waanachia Megawati 100 inaingia kwenye Grid ya Kenya lakini sio za kwao, hivyo Ethiopia anafunga mita mpakani mwake kati ya Kenya na Namanga pia itafungwa mita”, amesema.
Amesema chanzo cha umeme ni Ethiopia na malipo yatafanyika huko nan chi ya Kenya italipwa kiwango kidogo cha kutoa huduma ya kupitisha umeme.
Kuhusu kukamilika kwa Bwawa la Nyerere amesema makubaliano hayo yako pande mbili, kuna wakati Tanzania itachukua na kuna wakati nchi itapeleka ila hali ya kaskazini kwa sasa umeme utachukuliwa .