MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Profesa Mkenda Aitaka TAEC Kusomesha Watumishi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Profesa Mkenda Aitaka TAEC Kusomesha Watumishi
Habari

Profesa Mkenda Aitaka TAEC Kusomesha Watumishi

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda ameitaka Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), kusomesha watu wengi nje ya nchi kwa kuwa waliopo ni wachache.

Profesa Mkenda amesema hayo leo Februari 19,2025 alipokuwa akizindua Bodi ya TAEC, jijini Dar es Salaam.

“Tulikubaliana kuwapeleka watanzania kwenda kusoma kwenye vyuo bora duniani kwenye mambo ya atomu.

“Watu waliosoma katika atomu wako wachache sana hatuna watu wengi, tunahitaji wawe chuoni kufundisha na tunahitaji kuwa watendaji.

“Tungependa kazi mliyoanza ya kutenga fedha kwa ajili ya mafunzo ya muda mrefu ya vyuo vikuu nje ya nchi kazi hiyo iendeelee,” amesema Mkenda.

Mkenda amesema upo uwezekano mkubwa kwamba mionzi haijatumika kwa ufasaha katika eneo la tiba, kilimo na Kwenye viwanda.

Pia amesema japo kunakuwepo na ufadhili wa masomo, ila haupo kwenye maeneo yanayogusa mionzi, na kuipongeza tume hiyo kwa kutenga bajeti kwa ajili ya kuwapeleka watanzania nje ya nchi kwa ajili ya kujifunza mambo ya mionzi.

“Nawapongeza tume mmetenga bajeti kwa ajili ya kufundisha wa Tanzania nje ya nchi lazima tusisitize twende duniani tukajifunze katika vyuo bora tupeleke watanzania wakasome. Mlisimamie jambo hili kama bodi,” amesema na kuongeza kuwa mtanzania anaposoma vizuri anaisaidia nchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAEC, Profesa Najat Kassim Mohammed amesema tume hiyo inatekeleza majukumu ya kudhibiti na kuhamaisha matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia.

Amesema ili kuhakikisha bodi inatekeleza majukumu kwa usahihi kwa kushirikiana na Uongozi Institute wameandaa mafunzo maalum kwa uongozi wa bodi kuanzia Februari 17 hadi 21, 2025.

You Might Also Like

‘Viswaswadu’ kutumika kuboresha daftari la wapiga kura

Watafiti Watumia Mbinu Mpya Kudhibiti Mdudu Kantangaze Kwenye Nyanya Bila Viuatilifu

Chalamila: Serikali Imewekeza Kupatikana Wataalamu Wa Usingizi, Yapunguza Vifo Vinavyotokana Na Upasuaji

Rais Mwinyi Azindua Ripoti ya Jiolojia, Utafiti Madini zanzibar

TEA Kuhakikisha Mazingira Ya Kujifunzia, Kufundishia Yanaboreshwa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Nchimbi Agongelea Nyundo Kwa Wagombea Watoa Rushwa
Next Article Mpango Asema Tanzania, Korea Kubadilishana Wafanyakazi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Wadau Wakaribishwa Kuwekeza Katika Uchakataji, Biashara ya Mkonge Nchini
Habari August 7, 2025
Mramba Afungua Mafunzo Ya Teknolojia Ya Nishati Jua Kwa Watalaam
Habari August 7, 2025
Mbegu Bora za Miwa Zenye Tija ya Tani 200 kwa Hekta Zaendelea Kuwanufaisha Wakulima
Habari August 7, 2025
Mbegu Bora za Mpunga Zazalishwa TARI Dakawa, Ifakara
Habari August 7, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?