Na Lucy Lyatuu, Dodoma
MKUU wa mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amesema ofisi zote za mkoa huo ziko tayari kushirikiana na vyombo vya utangazaji nchini ili kurahisisha kazi na kuwezesha kazi zenye tija.
Amesema hayo leo katika mkutano wa mwaka wa vyombo vya utangazaji nchini unaofanyikankwa siku mbili katika mkoa wa Dodoma.
Amesema vyombo vya utangazaji vina ushirikiano kuufanya mkoa wa Dodoma kujulikana duniani ikwa kuandika na kutangaza yale mema ili kujulikana jambo litakaloleta maendeleo.
Amesema mkoa wa Dodoma unakua kwa kasi sana, na hilo limewezekana kutokana na jitihada za Rais Samia Suluhu Hassab kwani amewekeza kwa kiasi kikubwa kutoa heshima kwa watanzania kwa kuweka miradi mikubwa ya kimkakati ya kimakao makuu katika mkoa huo.
Amewashauri watangazaji kutokaikoabalimbali nchini waliokutana mkoani Dodoma kutembelea maeneo mbalimbali kuona kazi iliyofanywa na Rais Samia.
“Baadhi ya miradi ni iliyotekelezwa na Rais Samia ninpamoja na trenibya kisasa inayotumia umeme ya SGR, ukamilishwaji wa mji wa serikali, pamoja na mengi mengine, ” Amesema.
Amesema mbali ya miradi hiyo leo kuna mahakama ya makao makuu ambayo imekamilika ikiwa na jengo bora kwa Afrika pia ukamilishaji wa Chuo cha Ufundi cha Dodoma , Uwanja wa Ndege ikiwa ni miradi ya miradi ya kimkakati.