Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: WANAFUNZI wawili wakazi wa Vijibweni Kigamboni Mkoani Dar es Salaam, wamehojiwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kwamba wametekwa.
Kamanda Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema hayo alipozungumza na Waandishi wa Habari.
Muliro amesema Januari 29, mwaka huu liliwapata na kuwahoji wasichana wawili ambapo mmoja wa Miaka 16 Mwanafunzi wa Kidato cha Pili na mwingine Miaka 12 Mwanafunzi wa Darasa la saba kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo baada ya kutengeneza mazingira kuwa wametekwa na kwamba watekaji wanataka pesa.
“Ufutiliaji ulifanywa na kufanikiwa kubaini watoto hao walipokuwa na baada ya mahojiano ya kina walikiri kutengeneza tukio hilo la uongo ili waweze kujipatia
pesa kwa udanganyifu toka kwa wazazi wao baada ya kutoweka tarehe 26/01/2025 na kuelekea Longoni Beach ambapo walikesha hapo hadi tarehe
27/01/205 asubuhi.
“Na baadae kuelekea maeneo ya Tungi hadi walipokamatwa wakiwa wakizunguka. Jeshi linalaani vitendo hivyo vya watu vyenye lengo la kujipatia pesa kwa njia za udanganyifu,” amesema.