MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: SGR Kipande Cha Saba Na Nane kuanza kujengwa
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > SGR Kipande Cha Saba Na Nane kuanza kujengwa
Habari

SGR Kipande Cha Saba Na Nane kuanza kujengwa

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi

DAR ES SALAAM: SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC), limetiliana saini na Kampuni ya CREGC & CREDC Mkataba wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa  -SGR kutoka Uvinza Tanzania hadi Msongati Burundi.

Utiaji saini huo umeshuhudiwa na Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania  Makame Mbarawa pamoja na Waziri wa Miundombinu, Ardhi na Makazi wa Burundi.
Akizungumza wakati wa utiaji saini huo, Waziri Mbarawa amesema thamani ya ujenzi huo ni Sh. Trilioni 5.6.
Mbarawa amesema mradi huo una vipande viwili ambavyo ni kutoka Uvinza  mpaka Malagarasi, na kutoka Malagarasi hadi Msongati, jumla yake ikiwa ni Kilomita 282.
Waziri huyo ametoa maelekezo kwa TRC kuhakikisha mradi huo unafuata vigezo vya Kimataifa vya Usalama pia isimamie bajeti vizuri ili kuzuia gharama zisizokuwa za lazima.
Pia ameitaka TRC kushirikisha jamii mradi unaopita kwenye maeneo yao kwa kuwalipa fidia.
” Hakikisheni mnatoa fursa za ajira kwenye maeneo mradi unakopita,” amesema.
Naye Waziri wa miundombinu, Ardhi na Makazi nchini Burundi, Dieudonne Dukundane amesema uboreshaji wa huduma katika bandari ya Dar es Salaam na ujenzi wa reli hiyo ya kisasa, utainarisha uwekezaji sio kwa nchi hizo mbili tu, bali katika ukanda mzima.
Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba ameeleza kuwa fedha ya utekelezaji wa mradi huo ipo tayari, zilikuwa zinasubiri mjenzi apatikane.
“Reli ili iwe na tija ni lazima yote iwe imekamilika. Nitoe uhakika kwamba fedha kwa ajili ya vipengele vingine inakamilishwa. Ipo katika hatua za mwisho,” amesema.
Awali Mkurugenzi Mkuu TRC, Masanja Kadogosa ameshukuru utiaji saini huo wa kipande cha saba na cha nane ikiwa ni awamu ya pili ya mwendelezo wa reli ya kisasa.
Amesema ujenzi huo utachukua miezi 72, ukijumlisha kilomita 282, kilomita 240 zitakuwa za njia kuu na 42, njia za kupishana.
“Tutaendelea kusimamia kutimiza lengo la ujenzi unaotekeleza kwa viwango vilivyokusudiwa,” amesema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso ameshauri kipande kutoka Dodoma – Makutupora kwenda Tabora hadi Kigoma, kiende sambamba na ujenzi huo unaoanza.

You Might Also Like

Rais Samia awasili Zimbabwe

Daktari: Saratani ya Matiti Inazuilika, Inatibika

NIT Yajivunia Uanzishwaji Chuo Cha Marubani

Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu yaita wawekezaji

Kasulu Yaandaa Bonanza La Michezo Kuhamasisha Uchaguzi Mkuu, Mapokezi Ya Mwenge

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Sekta Binafsi Zazuia Wafanyakazi Kujiunga Na Vyama Vya Wafanyakazi
Next Article RC Chalamila Ataka Reli Za Ndani Ya Mkoa Kusafirisha Abiria, Kupunguza Msongamano
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?