MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TARI Yawafikia Wakulima Kilosa, Kilimo Shadidi Cha Mpunga
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TARI Yawafikia Wakulima Kilosa, Kilimo Shadidi Cha Mpunga
Habari

TARI Yawafikia Wakulima Kilosa, Kilimo Shadidi Cha Mpunga

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
MOROGORO: ZAIDI ya wakulima na maofisa ugani 2100 wamepatiwa elimu ya kanuni za kilimo shadidi cha mpunga kilichoboreshwa ili kuwawezesha kupata tija katika zao hilo.
Kilimo shadidi cha mpunga kinalenga kupunguza kiasi cha  matumizi ya mbegu, maji pamoja na tija kuongezeka.
Mratibu wa Mradi huo wa kilimo shadidi cha mpunga, kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Dkt. Atugonza Bilaro amesema idadi hiyo ya wakulima waliopata mafunzo hayo ni asilimia 108.8.
Dkt. Bilaro amesema mradi huo unatekelezwa katika, Halmashauri za Kilombero, Iringa, Chalinze, Bunda na Mbarali ambapo  baada ya kufikia malengo kwa sasa umetanua wigo wa kuwafikia Wakulima  katika Wilaya ya Kilosa,Morogoro.
Amesema TARI kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imeendelea na  mkakati wa kuboresha uzalishaji wa zao hilo, kwa wakulima na moafisa ugani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo ya Kilosa.
Bilaro amesema mafunzo hayo yamefanyika Disemba 17 hadi 21, 2024 kwa wakulima wa Skimu za Chanzuru, Rudewa, Ilonga, Kilangali na Mvumi ikiwa lengo ni kuwafikia wakulima 750 na maofisa ugani 10.
Naye Mkulima wa mpunga Skimu ya Chanzuru amesema miaka ya nyuma alipata mafunzo ya kilimo shadidi lakini ilikuwa  vigumu kuendelea kutekeleza kwa muda mrefu kutokana na changamoto za kung’oa miche wakati wa kupandikiza.
Mkulima Petro amesema  kupitia teknolojia ya Kitalu Mkeka aliyopata katika mafunzo hayo ni ya mafanikio sababu inajibu changamoto, hivyo kazi ya ung’oleaji itakuwa nyepesi.
Mradi huo unatekelezwa na  TARI kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti ya Norway- Norwegian Institute  of Bioeconomy research (NIBIO) na taasisi ya Utafiti ya Swamination (MSSRF) ya nchini India.

You Might Also Like

Bunge lapitisha muswada marekebisho ya sheria za Hifadhi ya Jamii

Watahiniwa 72 wa kidato cha nne wafutiwa mtihani kwa udanganyifu, kuandika lugha za matusi

Daktari: Saratani ya Matiti Inazuilika, Inatibika

Waajiri Wasilisheni Michango Kwa Wakati

Mikoa mitatu kuanzishwa vituo vya gesi asilia

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Polisi Kuimarisha Ulinzi Nyumba Za Ibada Krismasi, Mwaka Mpya
Next Article Tumeanza Kufanyia Kazi Maelekezo Ya Rais Samia – Bashungwa
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?