Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: KAMPUNI ya Ujenzi na Mawasiliano ya China (CCCC), imetoa vitabu 200 kwa maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo ya CCCC, Li Xuecai amesema wametoa msaada huo wa vitabu ikiwa ni mara ya pili sasa, mara ya kwanza ilikuwa mwaka jana.
Xuecai amesema utoaji huo wa vitabu hivyo chuoni hapo ni daraja la kuimarisha uhusiano kati ya China na Tanzania, pia ni sehemu ya kubadilishana utamduni baina ya nchi hizo mbili.

“Nashukuru kufikia tukio la kugawa vitabu kwa mara ya pili, mwaka jana pia tuligawa vitabu katika maktaba hii,” amesema,
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Maktaba chuoni hapo, Dkt. Collins Kimaryo ameshukuru kwa msaada huo na kusema vitabu walivyopokea ni vya sanaa, historia, sayansi na teknolojia.
” Vitabu vinagusa sanaa, historia, sayansi na teknolojia. Vinatufaa maana kazi za msingi ni kutoa huduma za machapisho mbalimbali.
” Vitabu tunavyopokea vitaongeza maarifa kwa wanafunzi, vitaongeza aina za majarida tuliyonayo, pia kuonyesha ushirikiano baina ya China na Tanzania, pia Chuo Kikuu na Kampuni hiyo,” amesema.
Kwa upande mwingine Mkurugenzi Mtanzania Taasisi ya Confucius, Profesa Aldin Mutembei ameishukuru kampuni hiyo kwa kutoa nakala hizo 200 chuoni hapo.

Amesema katika maktaba hiyo wanaendelea kujenga utamaduni baina ya Tanzania na China, pia kueleza watanzania namna gani nchi ya China inaendelea.
Mutembei amesema katika maktaba hiyo kuna vitabu
Vinavyozungumzia utawala na mawazo ya China, ameongeza usomaji wa vitabu unasaidia kuchagiza afya.