Na Mwandishi Wetu
VIJANA 26 kutoka vyuo vikuu mbalimbali wamekabidhiwa tiketi za safari za kwenda nchi za Ujerumani, Sweden, na Denmark kwa ajili ya programu za mafunzo kwa vitendo.

Akikabidhi tiketi hizo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete amesema programu hiyo inawezeshwa na Taasisi ya CRDB Bank Foundation kwa kushirikiana na Ushirika wa Wajasiriamali Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUGECO).
