MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Serikali  Kuja Na Mradi  Wa Kuimarisha Upatikanaji Umeme Vitongojini- Kapinga 
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Serikali  Kuja Na Mradi  Wa Kuimarisha Upatikanaji Umeme Vitongojini- Kapinga 
Habari

Serikali  Kuja Na Mradi  Wa Kuimarisha Upatikanaji Umeme Vitongojini- Kapinga 

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
GallaryNa  Mwandishi Wetu
NAIBU  Waziri wa Nishati,  Judith Kapinga amesema Serikali inatarajia kuanza mradi mpya wa upelekaji umeme  vitongojini utakaohusisha ujenzi wa njia za kati na ndogo za kusafirisha umeme.
 Kapinga ameyasema hayo leo Oktoba 31, 2024 bungeni jijini Dodoma  wakati akijibu swali la  George Mwanisongole, Mbunge wa Mbozi aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itaanza kupeleka umeme mkubwa kwenye Vitongoji ambavyo havijapata umeme mkubwa na hivyo kukosa sifa ya kuwepo kwenye miradi ya maendeleo.
“Kwenye mradi huu utakaoanza Desemba 2024 tumeboresha zaidi kwani tutakuwa na transfoma zenye ukubwa wa KVA 50, 100 na 200 kulingana na ukubwa wa Kitongoji.” Amesema Kapinga
Ameongeza kuwa, maeneo ya Vitongoji ambayo hayakunufaika na mradi wa awali wa vitongoji 15 yatanufaika kwa mradi utakaoanza Desemba 2024.
Akijibu swali la Mbunge wa Iringa Mjini, . Jesca Msambatavangu aliyeuliza ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya umeme jazilishi maeneo ya Miji yenye sura za Vijiji kama Ugele, Mosi, Cargrielo, Machinjio, Ulonge, Mtalagala na Msisina, Mhe. Kapinga amesema Serikali inaendelea kupeleka umeme katika maeneo ya vijijini yakiwemo maeneo ya Miji yenye sura za Vijiji.
 Aidha, kwa maeneo ya Ugele, Mosi, Cargrielo, Machinjio, Ulonge, Mtalagala na Msisina yaliyopo katika Jimbo la Iringa Mjini, Serikali itayapelekea umeme kupitia mradi wa kupeleka umeme katika Vitongoji 15 kwa kila Jimbo.
Ameongeza kuwa, maeneo ya Cargrielo na Machinjio  yatapatiwa umeme na TANESCO kupitia miradi yake ya ndani ya kusogeza miundombinu ya umeme kwa wananchi.

You Might Also Like

Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar

VETA Shinyanga Yatumia Kompyuta Kubuni Bidhaa 

TEA, UNICEF na Canada waendeleza mageuzi ya elimu Sikonge

Huduma ya Mahakama ya Mwanzo yasogezwa Wilaya ya Ubungo

Midea Group Yafungua Duka Mlimani City Dar Es Salaam

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Spika Ahoji Mwongozo Wa Wanaojitolea Kazin
Next Article REA Yatoa Kipaumbele Ujenzi Miradi Ya Nishati Jadidifu
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
Viongozi Wa Dini Zote Wajifungie Kuomba,Kujadili Na Kutoa Mapendekezo-SAU
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?