MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Miaka 60 Mikumi na mapinduzi makubwa sekta ya utalii
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Miaka 60 Mikumi na mapinduzi makubwa sekta ya utalii
Habari

Miaka 60 Mikumi na mapinduzi makubwa sekta ya utalii

Author
By Author
Share
4 Min Read
Na Mwandishi wetu
Miaka 60 ya kuanzishwa kwa Hifadhi ya Taifa Mikumi imeleta mafanikio makubwa katika Sekta ya Utalii nchini yakichangiwa na jitihada zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Hayo yamesemwa  leo Agosti 31,2024 na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Pindi Chana  wakati wa Maadhimisho ya Miaka 60 ya Hifadhi ya Taifa Mikumi mkoani Morogoro.
Amesema  kupitia filamu maarufu ya “Tanzania: The Royal Tour” pamoja na filamu ya “The Amazing TANZANIA”zimekuwa chachu ya kukuza utalii na kuongeza idadi ya wageni wa ndani na nje ya nchi.
“Kufuatia jitihada hizo za Rais Samia, katika mwaka wa fedha 2023/2024 idadi ya watalii wa kimataifa waliofika nchini imeongezeka kwa asilimia 96 kutoka watalii 922,692 Mwaka 2021 hadi kufikia watalii 1,808,205 Mwaka 2023” amesema.
Pia amesema upande wa Hifadhi ya Taifa Mikumi, kwa mwaka 2023/2024 jumla ya watalii 138,844 wametembelea Hifadhi hiyo sawa na ongezeko la asilimia 198.48 kutoka watalii 46,517 waliotembelea hifadhi hiyo kwa mwaka 2020/2021.
Ameongeza kuwa Serikali imeendelea kuimarisha huduma kwa watalii kwa kuboresha miundombinu ya utalii ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa ya mwendokasi (SGR), kuimarisha Shirika la Ndege nchini (ATCL) na ujenzi wa barabara kurahisisha watalii kufikia vivutio mbalimbali.
Katika kuboresha miundombinu ya utalii ndani ya Hifadhi ya Taifa Mikumi, Serikali kupitia Mradi wa REGROW inaboresha uwanja wa ndege kuwa wa kisasa katika eneo la Kikoboga,
Pia ujenzi wa malango ya watalii eneo la Doma na Kikwaraza, ujenzi wa kituo cha kutoa taarifa kwa wageni, kambi za kupumzikia wageni.  maeneo ya malazi na kuunganisha Hifadhi ya Taifa Mikumi kwenye umeme wa Gridi ya Taifa.
Amesema miradi hiyo itakapokamilika itawezesha kuongeza idadi ya watalii kwa kuwa ndege kubwa zaidi zitaweza kutua ndani ya Hifadhi ya Taifa Mikumi ambapo kwa wakati mmoja wageni zaidi ya 140 wataweza kuhudumiwa kwa pamoja.
Pia, amesema Serikali imepanga kujenga lango la kupokelea watalii watakaokuja Mikumi kwa njia ya reli ya ya kisasa ya mwendokasi (SGR) kupitia kituo cha reli ya SGR kilichopo kwenye mji wa Kilosa. Ujenzi wa lango hili utaleta chachu ya maendeleo kwa wananchi wa Wilaya Kilosa hususan kwa vijiji vya Myombo, Mbamba na Kilangali.
Naye, Kamishna wa Uhifadhi Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Musa Kuji amesema kuwa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi ilikua ikishika nafasi ya 14 kati ya hifadhi 21 katika ukusanyaji wa mapato ambapo kwa sasa iinashika nafasi ya 6.
Kwa upande wake Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Mikumi, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Augustine Massesa  amesema kupitia utalii wa Hifadhi ya Taifa Mikumi uchumi wa jamii zinazozunguka eneo hilo umeongezeka
Kwani wameweza kushirikiana na jamii kuwapa fursa za ajira, elimu ya uhifadhi, miradi ya maendeleo pamoja na kushirikiana na Askari wa Vijiji (VGS) kukabiliana na changamoto ya Wanyamapori wakali na waharibifu.
Hifadhi hii ni hifadhi kongwe ambayo ni Hifadhi ya Taifa ya tano kuanzishwa baada ya Hifadhi za Taifa za Serengeti (1951), Ziwa Manyara (1960), Arusha (1960) na Ruaha (1964). inaadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1964 kwa Tangazo la Serikali Na 465.

You Might Also Like

OSHA Yatoa Gawio Kwa Serikali Zaidi  Ya Bilioni 10

PIC Uwekezaji Bidhaa Za Ngozi Utaongeza Mapato

Mpogolo Aipongeza Halmashauri Maandalizi Mikopo Asilimia 10

RC Serukamba Aiunga Mkono REAUgawaji Wa Mitungi Ya Gesi Iringa

TTCL Yafanya Maboresho Makubwa Kwa Watumiaji

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais Samia Suluhu Hassan, kuongoza Kamati Kuu Maalum kesho
Next Article Rais Samia akagua gwaride maalum
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Nyanya Cheri na Ngogwe Chungu Zarejea 
Habari July 13, 2025
NFRA Yawaalika Wadau Kununua Nafaka kwa Masoko ya Ndani na Nje
Habari July 13, 2025
Kafulila: Ushirikiano wa Sekta Binafsi na Umma Kuboresha Huduma
Habari July 13, 2025
Teknolojia Mpya Ya Uchomeleaji Yaleta Mapinduzi VETA Dodoma
Habari July 12, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?