Lucy Lyatuu
MKUTANO wa nane wa mawaziri wa Uvuvi,Bahari na maji ukanda wa karibiani na pasifiki (OACPS) unatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam ukilenga kuweka mkakati wa pamoja kuhusiana na sera zinazohusiana na masuala ya Uvuvi na ufugaji pamoja na viumbe maji.
Mkutabo huo unatarajia kufanyika kuanzia Septemba 9 mpaka 13 mwaka 2024 ukijumuisha mawaziri wakisekta, wataalam wa sekta ya Uvuvi kutoka nchi wanachamana na ulimwengu Kwa ujumla, Taasisi sisizo za kiserikali, Taasisi za kikanda,watafiti,vyuo vikuu,na Wavuvi wadogo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema hayo Leo alipozungumza na waandishi wa habari kuelekea mkutano huo na kwamba Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi .
Amesema mkutano huo umepangwa kufanyika pamoja na kongamano la kimataifa kuhusu mikakati ya uboreshaji wa mnyororo wa uzalishaji wa vyakula vya majini.
Kuhusu lengo la mkutano huo Waziri Ulega amesema ni kujadili masuala mbalimbali ya sekta ya Uvuvi katika nchi wanachamana ikiwa ni pamoja na kuweka mkakati wa pamojas kuhusiana na sera zinazohusiana na masuala ya Uvuvi na ufugaji viumbe maji Ili Kuimarisha sekta ya Uvuvi.
Amesema pamoja na hayo ameeleza manufaa yatakayopatikana kuwa ni kufungua fursa za uwekezaji kwenye uchumi wa bluu hususani kwenye maeneo makuu mawili ya Uvuvi na Ufugaji samaki, pamoja na kuendelea kuboresha mahusiano ya matumizi ya rasilimali za maji ya asili.
Mkutano huo utafungwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi