Na Mwandishi Wetu
RAIS Samia Suluhu Hassan amekabidhi vyeti vya kutambua mchango wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), kwa ajili ya kutambua mchango wao kwa jamii.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete amesema hayo.

“Nimepokea vyeti vya kutambua mchango wa Mashirika yetu mawili NSSF na WCF kwa mchango wao katika kurudisha kwa jamii.
“Vyeti hivyo vimetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan,”amesema.
Amesema vyeti hivyo vimetolewa na Rais Samia kwa kuwa, mashirika hayo yamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha yanajenga na kuwezesha jamii kujitegemea.
Amesema kupitia kazi zao na mapato yao, jamii imeendelea kufaidia kwa matokeo mbalimbali ususani uwekezaji unaofanyika.