MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Baraza la uuguzi na ukunga lawakaribisha wenye malalamiko
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Baraza la uuguzi na ukunga lawakaribisha wenye malalamiko
Habari

Baraza la uuguzi na ukunga lawakaribisha wenye malalamiko

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: BARAZA la Uuguzi na Ukunga Tanzania, limesema endapo mgonjwa atakuwa hajaridhika baada ya kufikisha malalamiko yake katika Kituo cha Afya  hadi mkoa, basi afike katika baraza hilo.
Ofisa Habari na Mawasiliano wa baraza hilo, Ndimnyake Mwakapiso amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi yanayoendelea jijini Dodoma.
Amesema, “Kwa wenye malalamiko kama kuna mgonjwa hakutendewa sawasawa  kuna ngazi ya malalamiko kuanzia kituo cha afya hadi mkoa na kama hajaridhika anaweza kwenda Baraza la Ukunga na uuguzi kupeleka malalamiko,”.
Amesema mara nyingi kupitia maonesho mbalimbali wamekuwa wakielimisha wananchi kupitia njia mbalimbali ili wananchi wajue baraza hilo ni chombo chao cha kufikishia kero wanapokuwa na shida.
Amesema baraza hilo linasimamia taaluma ya uuguzi na ukunga kuhakikisha kundi hilo kubwa la watoa huduma kwa kufuata misingi, taratibu, miiko, kanuni na sheria.
“Yapo majukumu mengi ambayo baraza linafanya, moja kati ya majukumu makuu ni kumshauri waziri wa Afya kuruhusu masuala yote ya sera ya uuguzi na ukunga, kama kuna marekebisho, kuna kitu cha kuongeza,” amesema.
Amesema baraza hilo ni muhimu kwa kuwa chuo hakiwezi kutoa taaluma ya uuguzi au ukunga bila kusajiliwa na baraza hilo.
Katika hatua nyingine, amesema mwaka jana wa fedha kulikuwa na mashauri takribani 26 ambayo waliyapokea, hivyo wapo wahusika waliopewa onyo na wengine kusimamishwa kazi miaka miwili.

You Might Also Like

Bodi ya mkonge kutoa ajira kwa watu 10,000 ifukapo 2030

Trump Ashinda Uchaguzi Marekani

Kituo Cha Mkutano Cha Kimataifa Mlima Kilimanjaro Kuileta Dunia Tanzania

Kingalame Aitaka Sekta Binafsi Kushirikiana na TBA Kukamilisha Mradi wa Makazi Geita

Ntonda Ameipongeza TEA Kwa Utekelezaji Bora Wa Miradi Ya Elimu

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TPHPA yafundisha namna sahihi ya utumiaji wa viuatilifu
Next Article Limeni mkonge unalipa – Maghali
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?