Na Mwandishi Wetu – Zambia
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani Kanda ya Afrika, Elcia Grandcourt, ambapo wamejadili kuendeleza ushirikiano na Shirika hilo hususan, fursa na programu mbalimbali katika maeneo ya uendelezaji wa mazao ya utalii.
Maeneo mengine ni utangazaji utalii, kuvutia uwekezaji katika miundombinu ya utalii na huduma, utoaji wa mafunzo na kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya utalii.
Kikao hicho kilimefanyika leo katika Hoteli ya Avani Victoria Falls Resort, Jijini Livingstone Zambia na kuhudhuriwa na Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kitaalam wa UN, Jaime Mayaki, Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Richie Wandwi pamoja na Ofisa Utalii wa UN Tourism, Bi. Zineb Remmal.