Na Lucy Lyatuu
DAR ES SALAAM: SERIKALI imewataka wadau wa usafirishaji kuzingatia maslahi ya wafamyakazi wao kwani yapo malalamiko kutoka Kwa wafanyakazi kutotendewa haki.
Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile amesema hayo Dar es Salaam katika jukwaa lililoandaliwa na Taasis ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili pamoja na kuzitafutia suluhisho.
Akizungumza baada ya kusikiliza changamoto za Sekta hiyo, Kihenzile amesema pamoja na mambo mengine lakini wadau hao wajitahidi kutenda haki kwa wafanyakazi wao ikiwa ni pamoja na kuwalipa inavyostahili.
Kumbukeni kuwepo kwenye hizo nafasi ni Kwa neema ya Mungu tu..watendeeni vyema mkijua kuwa yapo malipo mbele ya haki,” amesema Kihenzile na kuwataka pia kutambua mageuzi ya uboreshaji wa sekta hiyo yanayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Kuhusu mageuzi Kwa sekta hiyo amesema ni Vizuri kuelewa nchi inakoelekea,na kujipanga namna ya kufikia fursa zilizopo katika sekta hiyo.
Kihenzile amesema eneo lingine linaloangaliwa Kwa maboresho ni kwenye kujenga bandari kavu katika eneo la Tunduma ambapo tayari imemepata ekari 6000 lengo kuondoa msongamano wa malori ya mizigo.
Hata hivyo alitoa wito kwa taasisi za fedha kushusha riba na kuwakopesha wadau wa sekta hiyo Ili kuzifikia fursa mbalimbali lengo likiwa ni kukuza uchumi na hata kuongeza ajira.
Awali akizungumza Mtendaji Mkuu wa TPSF, Rafael Maganga amesema taasisi hiyo inaadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa ikiwa na lengo kukuza uchumi kufika dira ya maendeleo 2050.
Amesema kongamano limewaleta pamoja wadau mbalimbali wa maendeleo Ili kujadili changamoto zinazoathiri ufanisi wa sekta hiyo na kuwataka kutoa mapendekezo yao.
“Michango wa sekta unakuwa Kwa asilimia nane na inaumganisha sekta zote nchini,hivyo changamoto zilizopo ziweze kufanyiwa kazi,” amesema.