Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 6, 2026
Habari Lucy Ngowi 10

GCLA Yaimarisha Udhibiti Wa Kemikali Katika Uchimbaji Wa Madini

Na Lucy Ngowi
GEITA: MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) imeeleza kuwa inaendelea kuimarisha usimamizi na udhibiti wa matumizi ya kemikali nchini, hususan katika shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini, kwa lengo la kulinda afya za watu na mazingira.
Akizungumza kuhusu majukumu ya mamlaka hiyo, Meneja wa Kanda ya Ziwa wa GCLA, John Faustine, amesema mamlaka hiyo inasimamia sheria tatu kuu, ikiwemo sheria inayohusu usimamizi na udhibiti wa kemikali za viwandani na majumbani.
Amesema Mkemia Mkuu wa Serikali ndiye msajili wa kemikali nchini, akihusika na usajili wa wadau, kemikali pamoja na maeneo yanayotumia kemikali hizo.
Faustine amesema GCLA pia hufanya ukaguzi na kutoa elimu kwa watumiaji kuhusu matumizi sahihi na salama ya kemikali ili kupunguza madhara kwa afya, jamii na mazingira.
Kwa upande wa maabara, amesema GCLA ina maabara zenye ithibati na vifaa vya kisasa vinavyosaidia wachimbaji kubaini uwepo na ubora wa madini, pamoja na kutambua madini shindani yanayoweza kujitokeza wakati wa uchenjuaji.
Aidha, amesema Mkemia Mkuu wa Serikali husajili maabara za kemikali na sayansi jinai ili kuhakikisha zinatoa majibu sahihi na ya kuaminika kwa wakati.
Kuhusu tiba asili, amesema GCLA hushirikiana na Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala kupima usalama, ubora na viambata vya sumu katika dawa zinazotokana na mimea.
Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.